Na John Walter-Manyara
Basi
la abiria kampuni ya Mohamed Classic lenye namba T 643 DJP lililokuwa
linatoka Arusha kwenda Kigoma limepata ajali ya kugongana na Fusso lenye
namba T 380 DWF iliyokuwa inatokaTabora kwenda Moshi na kusababisha
vifo vya watu wa 3 na majeruhi 26.
Ajali hiyo imetokea leo tarehe 24/5/2022 wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.
Akizungumza
kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga amesema ajali hiyo
imesababisha vifo vya watu 2 kwenye basi na kifo cha mtu 1 kwenye fuso
pamoja na kusababisha majeruhi 26 ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo
ni uzembe wa dereva wa basi kutokuheshimu alama za barabarani.
Hata hivyo jeshi hilo linamtafuta dereva wa basi hilo ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.
Majeruhi
katika ajali hiyo, wanaume ni 14, wanawake 10 pamoja na watoto 2 ambao
wamefikishwa katika Hospitali ya Tumaini, wilaya Hanang Mkoani Manyara.
Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa watumishi wa barabara kuzingatia sheria za usalama Barabarani ili kuepukana na ajali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...