MBUNGE wa Jimbo la Kojani , Wilaya ya Wete , Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hamad Hassan Chande, amekutana na kuzungmza na wananchi wake waishio Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuwapa mikakati ya maendeleo katika jimbo hilo.

mewataka wananchi wa jimbo hilo kuwa na imani naye kwani anamikakati mikubwa ya kuleta maendeleo.

Amesema, katika kutatua changamoto k jimboni humo, ameunda timu iliyofanya utafiti wa kina wa kubaini changamoto na kutoa suluhisho, hatua ambayo itarahisisha kasi ya maendeleo.

Kuhusu sekta ya Uvuvi, Chande amewatangazia neema wavuvi kutoka Kojani kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameagiza maboti 500 ambayo anayagawa kwa wavuvi kupitia Mkakati wa Uchumi wa Buluu.

Amesema katika awamu iliyopita ya ugawaji maboti hayo Kojani haikopata lakini awamu hii Rais Dk. Mwinyi amemhakikishia kuwa Kojani atapata mgao mkubwa zaidi.

“Niliongea na Rais Dk. Mwinyi, alinihakikishia kuwa katika maboti hayo 500 yatakayo kuja Kojani tutapata mgao wa asilimia 15. Muwe na imani na Rais wetu kwa sababu ni mcha Mungu na msikivu. Hili atalitekeleza,”ameeleza.

Pia ametanabaisha kuwa , serikali ni sikivu hivyo changamoto zote za wavuvi wa Kojani ataziwasilisha katika mamlaka husika kwani jimbo hilo ndiyo kitovu cha uvuvi.

Hata hivyo aliwataka wavuvi kuwa wakweli, kuheshimu sheria za nchi na kushughulikia changamoto zao kw kufuata taratibu.

Kwa upande wa sekta ya elimu, Chande ameeleza tayari ameanza kuchukua hatua ambapo ameandaa madawati 500 ambayo yatasambazwa shuleni.

Ameahidi hidi kushughuliia uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi, maadalizi na sekondari

“Mimi nilikuwa mwalimu Kojani. Natambua changamoto zote za elimu zilizopo. Kuna uhaba wa madarasa nane katika shule za msingi na madarasa mawili kwa shule za maandalizi,”amesema.

Ameongeza hatua zinaendelea kufanyika ili kujenga madarasa hayo.

Katika kukabiliana na uhaba wa walimu, Chande, ameeleza kuwa ametafuta walimu 10 kutoka mkoani Morogoro ambao watapelekwa Kojani na atakuwa akiwagharamia yeye isipokkuwa marazi.

Kuhuse sekta ya afya, Chande alisema bado kuna changamoto hasa ya wataalamu, ikiwemo kada ya wafamasia.

Katika kushughulikia hilo ametafuta wafamasia watatu ambao watapelekwa Kojani kwani hivi sasa wauguz i ndiyo hutoa dawa jambo ambalo siyo sahihi.

“Pia niko katika harakata kutafuta magar mawili ya kubebea wagonjwa. Japani wameahidi kunipa boti ya kisasa ya kubebea wagonjwa, hivyo tutapunguza changamoto,” ameeleza Mbunge huyo.

Amehimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki sense ya watu na makazi kwani kuto kuhesabiwa ni sawa na kudhurumu haki za wengine.

Awali Katibu wa Ofisi ya Mbunge Said Shaame Hamis, amewataka wananchi wa Kojani kushikamana na kuto kuruhusu kugawanywa kwa tofauti ya itikadi za kisiasa.

“Tushirikiane kikamilifu na Mbunge wetu. Atatufikisha mbali. Katika kipindi kifupi amefanya mambo mengi mazuri,”ameelleza.

Katika lisara yao wananchi hao wa Kojani, wamempongeza mbunge huyo kwa kuona umuhimu wa kukutana nao nje ya jimbo ambalo walidai halijawahi kufanywa na kiongozi yoyo kutoka katika jimbo hilo. Pia wamewasilisha chamoto mbalimbali zikiwemo za ellimu, afya, ajira, kuto kuthaminiwa kwa sekta ya uvuvi pamoja na sheria inayo wabana.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...