Na Mwandishi Wetu
MWANAFUNZI wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Sandra Sommi kozi ya Uhandisi wa Komputa leo ameibuka mshindi wa kwanza katika kundi la vyuo vya kati katika mashindano ya Kimataifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU 2022).
Ushindi wa Sandra unatoka na ubunifu wake wa mashine ya kumsaidia watoto chini ya miaka mitano kupumua (bable CPAP).
Mshindi huyo amekabidhiwa na Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango hundi ya Sh milioni tano na cheti.
Dkt. Mpango alikua mgeni rasmi katika hafla ya kufunga maonesho hayo ya Kilele cha Wiki ya Ubunifu Kimataifa yanayofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Jamhuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...