Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa 33 wa APRA na kueleza kuwa hiyo ni fursa kwa Taifa kujifunza kutoka nchi nyingine na ni nafasi ya kutangaza vivtio vya utalii, Leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Maofisa Uhusiano Afrika (APRA,) Yomi Okusanya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo na kueleza kuwa mkutano huo utawaweka pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazolikumba bara la Afrika na nafasi ya vyombo vya habari katika kuleta suluhisho.





NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amewataka wadau wa sekta ya habari na mawasiliano nchini kutumia fursa ya uwepo wa maofisa uhusiano na wadau wa sekta hiyo kutoka mataifa mbalimbali, kuimarisha mfumo wa utoaji habari na mawasiliano maeneo yao ya kazi


Kundo ameyasema hayo leo Mei 24, 2022 katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maofisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka nchi zipatazo 21 barani Afrika (APRA,) na nchi za Bulgaria na Marekani na mkutano huo utafanyika kuanzia leo hadi Mei 27 mwezi huu jijini Dar es Salaam.


Amesema kuwa, kutano huo uliobeba kauli mbiu ya ''One Africa, We Bring Africa in Tanzania'' umebeba matukio muhimu ya kupaisha Taifa ikiwemo kukutana na wanafunzi wanaosomea fani za uhusiano kwa Umma na kuwaeleza fursa zilizopo nje ya mipaka ya Tanzania, mkutano wa wanachama na usiku wa Tanzania Night ambao ni kwa ajili ya kutangaza vivutio vya taifa na kuwataka wenyeji kujipambanua vyema kama Rais Samia alivyoonesha mfano kupitia Royal Tour.


Amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini, ni fursa kwa Watanzania na utazidi kufungua milango zaidi kwa wawekezaji kwenye sekta ya habari na mawasiliano pia itamarisha mifumo ya upatikanaji wa habari kutoka kwa maofisa uhusiano na mawasiliano nchini.


Amewataka Maofisa hao kujikita katika kuchukua ujuzi wenye tija hasa juu ya namna ya kulisemea vyema Taifa ili kuikuza sekta ya habari nchini pamoja na kutangaza viivutio vya utalii vinavyopatikana nchini kwa wageni.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Maofisa Uhusiano Afrika (APRA,) Yomi Okusanya ameeleza kuwa mkutano huo utawaweka pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazolikumba bara la Afrika na nafasi ya vyombo vya habari katika kuleta suluhisho.


Amesema watakuwa na mikutano mbalimbali itakayohusisha Serikali ya Tanzania ambapo watajadili kwa pamoja na kuweka maazimio ili kulijenga bara la Afrika kwa ujumla na kueleza kuwa watakutana na wanafunzi wanaosoma taaluma ya habari na kuwapa uzoefu juu ya taaluma hiyo.


Mkutano huo wa 33 wa Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Afrika umelenga kujadili changamoto mbalimbali katika sekta hiyo na una washiriki kutoka zaidi ya mataifa 20 Afrika.



Mjadala ukiendelea.






Matukio mbalimbali katika ufunguzi wa mkutano huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...