Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Lindi

MBUNGE wa Jimbo la Mtamba ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mapenzi makubwa aliyonayo kwa wananchi hasa ya kuleta maendeleo katika kila sekta.

Nape ameyasema hayo leo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Lindi waliohudhuria tukio la aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 Bernard Membe kukabidhiwa kadi ya uanachama wa CCM baada ya kurejea tena kwenye chama hicho.

Akielezea zaidi ,Nape amesema katika jimbo la Mtama ambalo ameanza kulitumikia mwaka 2015 kuna mambo mengi yalikuwa yamekwama kwasababu za kisiasa lakini Rais Samia amefungua milango na sasa mambo yanakwenda vizuri.

“Vijiji vingi kwenye tarafa yetu vilikuwa havina umeme lakini leo hii vijiji vyote chini ya Rais Samia tumepata umeme,  kila kilichokuwa kimekwama sasa kinatekelezwa tena kwa kasi.Katika sekta ya afya  hospitali ya Rondo nayo itamaliziwa na ianze kufanya kazi.

“Tumepokea Sh.bilioni 2.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji, chini ya uongozi wa mama Samia mambo yanakwenda vizuri.Rondo barabara zilikuwa zimefungwa lakini Rais Samia ametoa fedha, tunajenga barabara kutoka Nyengedi kwenda Tamba.

“Miaka mitano iliyopita tulikuwa tunapata wastani wa Sh.milioni 400 za barabara  na wakati mwingine tunagawana  wenzetu wa Mchinga lakini chini ya Mama Samia ameleta zaidi ya Sh.bilioni tatu kwa ajili ya barabara, wasiomuelewa Rais Samia tunawaambia sisi tunamuelewa,”amesema Nape.

Aidha amesema katika Jimbo la Mtama asilimia 80 ni wakulima wa korosho na tayari Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeshatoa fedha kwa ajili ya kugawa pembejeo bure.

“Rais ameokoa wakulima Kusini ambao wengi wao ni wakulima wa korosho.Ukindoa fedha hizo hapa Chiponda tunamuelewa sana Rais Samia kwani watoto walikuwa wanatembea kutoka hapa kwenda kusoma Mnara Sekondari.

“Tulitengeneza shule lakini ikaingia siasa .Rais Samia amesikia kilio chetu ameleta fedha na shule inajengwa.Wana Chiponda , wana Rondo wanamuelewa Mama kwasasabababu watoto wao watasoma hapa.

“Najua kuna  shida ya mawasiliano na mimi ndio Waziri wa Mawasiliano , hivyo hakuna shida.Kikubwa tunasema tunamshukuru Mama amerudishia heshima ,amerudisha upendo.Mama ametulete matumaini, mwaka 2025 Rais Samia akachukue fomu, wala asiwe na wasiwasi,”amesema Nape.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...