Njombe
Mahakama
ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imemsomea shtaka la ulawiti
ndugu,Bahati Langson Sanga (36) mkazi wa kijiji cha Ihanga kata ya
Ukwama anayetuhumiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto.
Imeelezwa
kuwa mnamo tarehe 17 Aprili 2022 katika kijiji cha Ihanga mshtakiwa
alitenda kosa hilo la kumlawiti mtoto kinyume na kifungu cha 154 (1)a
ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo 2019.
Hata hivyo amesomewa shtaka lake na kukanusha kutenda kosa hilo.
Shauri
hilo limeongozwa na hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Makete Mh.Ivan
Msaki pamoja na mwendesha mashtaka ambaye ni Inspecta wa jeshi la
Polisi Benstard Mwoshe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...