Na Pamela Mollel,Arusha

Mamlaka ya manunuzi ya umma nchini  PPRA wametakiwa kusimamia na kufanya ukaguzi wa manunuzi na Ugavi wa bidhaa mbali mbali  za miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini ili kutumia fedha za walipa kodi kikamilifu.

Kauli hiyo ameitoa Mstahiki meya wa jiji la Arusha Maximilian Iranqhe  kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella wakati akifunga kongamano la wiki ya ununuzi wa umma  jijini Arusha ambapo ameleza ununuzi nimuhimu uzingatie misingi na uadilifu wa fedha za umma na kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

"Niwaombe waadilifu katika kusimamia manunuzi ya umma kupitia miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini kwa lengo la kuokoa fedha za serikali za walipa kodi kwa ni kwa kufanya hivyo thamani ya fedha itaonekana kupitia bidhaa husika,"amesema Iraqhe.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya ununuzi wa umma na afisa mtendaji mkuu wa PPRA Dkt Irene  Isaack amesema katika kongamano hilo wameazimia maazimio 11 yaliolenga katika ununuzi na kuongeza tija katika serikali sambamba na kufufanya tasmini kabla ya manunuzi

Dkt.Isaka amesema maazimio hayo yanalenga katika suala zima la uadilifu katika ununuzi wa umma ambao unaupunguzia gharama ya manunuzi katika serikali ikiwa lengo ni kuongeza tija pamoja na kuokoa fedha za walipa kodi za watanzania.

"Kwa hiyo kuna maazimio kwa upande wa mifumo ambayo inahitaji kufanya manunuzi kwa kutumia mifumo kuepuka matumizi ya kila taasisi kujiundia mifumo yao hivyo serikali mtandao imetakiwa kuhakikisha mifumo hiyo inazungumza,"amesema Mtendaji Mkuu.

Pia amesema maelekezo mengine ni pamoja ya kufanya tathmini ya kutosha kabla ya kufanya manunuzi ili kuepuka kununua bidhaa kwa gharama mara mbili ya ile ambayo iliyokusudiwa.

Kwa upende wake Kaimu Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) Cairo mwaitete katika kuangalia manunuzi ya umma ni lazima yaambatane na maadili hiyo kupitia hilo ni wajibu wao kama chuo kuwaandaa vijana kuzingatia weledi na maadili ya manunuzi.

 "Maadili ndio suala la msingi linaonyesha thamani ya fedha hivyo ni vyema tukajitahidi katika suala la manunuzi tuweze kuwaandaa vijana watakaokuwa na maadili ya manunuzi ikiwa sehemu kubwa ya bajeti ya Taifa kwa asilimia 80 ni manunuzi tu,"amesema Mkuu huyo.

Mtendaji Mkuu PPRA,Dkt.Irene Isaka
Kaimu Mkuu wa chuo cha uhasibu,Dkt.Cairo Mwaitete akizungumza na vyombo vya habari

Meya wa jiji la Arusha,Maximilian Iranqhe akifunga mkutano wa PPRA akimuakilisha mkuu wa Mkoa wa Arusha

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...