Mkuu wa Mkoa Pwani Mhe.
Abubakar Kunenge amewataka watalaam wa afya Mkoani hapo kutumia
utaalamu wao na kuja na Mikakati ili kuleta matokeo katika kupunguza
vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Kunenge
ameyasema hayo Mei 30, 2022 wakati akifungua kikao kazi cha Wataalamu
na Wadau wa Utekelezaji wa Mradi wa KOFIH Wilayani Bagamoyo ukumbi wa
Millennium beach Resort
Kunenge amewataka Wataalamu hao kushirikisha Wananchi katika uaandaaji wa mipango yao.
"Lazima mjipange mumize Vichwa tupate Mikakati yenye matokeo chanya" alisema Kunenge.Kunenge
amewaeleza kuwa tayari "Matarajio yanafahamika katika Sera na ilani ya
chama cha mapinduzi nini kifanyike kufikia malengo hayo ni kazi yenu
Wataalamu" alisema Kunenge.
Kunenge
ameeleza kuwa kupitia mradi huo Mkoa umeweza kupunguza Vito vya akina
mama vitokanavyo na uzazi toka 82 mwaka 2015 hadi 51 mwaka 2021 na vifo
vya watoto wachanga vimepungua kutoka 887 mwaka 2015 hadi 392 mwaka
2021.
Kunenge
amewashukuru wadau hao kuwa kuongeza mwaka mmoja wa Mradi na kufanya
mradi huu kuwa wa miakw 7 na wameongeza kiasi cha pesa toka dola za
kimarekani 3,000,000 kufikia dola 4,900,000.
Awali
akizungumzia faida mbalimbali zilizotokana na mradi wa KOFIH Mkoani
Pwani mganga mkuu Dr Guni Kamba amesema wameweza kupata mafunzo
mbalimbali ikiwemo ya Wataalam watoa dawa za usingizi, Ujenzi wa vyumba
vya upasuaji, vifaa tiba, ambulance na kujengewa wadi za wagonjwa,
Pia mwakilishi wa wizara Dr.Phineas sospiter amelishukuru Mradi wa KOFIH Kwa kuisadia wizara kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Naye
Mr Seungrae Ha Mwakilishi KOFIH Tanzania amesema kwa pamoja tumeweza
kukuza huduma za Afya Tanzania, na wamekutana kwenye kikao hicho kufanya
Tathimin ya Mradi kwa miaka 6 iliyopita na kupanga mipango ya
Utekelezaji kwa mwaka ujao.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na madaktar Wakuu wa Wilaya timu za usimamizi wa
Afya za Wilaya wawakilishi kutoka Mikoa ya Pwani, Dodoma na Morogoro.
Kwa Mkoa wa Pwani Mradi huu unatekelezwa katika Halmshauri 6 za Mkoa huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...