Na Humphrey Shao, Michuzi Tv 

Imebainika kuwa kati ya wakazi wa milioni tano wanaoishi mkoa wa Dar es salaam ni watu milioni na nusu ndio mwenye ajira iwe ya kujiajiri au ya kuajiriwa huku jitihada za makusudi zikihitajika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira.

Hayo yamebainishwa leo,ji wa matokeo y kaimu meneja wa takwimu za ajira na bei kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu,James Mbongo,wakati wa usambazaa Utafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2020 na 2021 kwa Kanda ya Mashariki.

Mbongo amesema katika utafiti huo inaonesha bado kuna tatizo la ajira na Mkoa wa Dar es unatajwa kuwa na changamoto kubwa ya tatizo la ajira tofauti na maeneo mengine na kuwataka watendaji wa kata kwenda kutatua changamoto hiyo kwa kuibua miradi mbalimbali.

Aidha,Mbongo amesema katika tafiti hiyo imeonesha asilimia 69 ya wanawake katika mkoa wa Dar es salaam hawana kazi huku pia tafiti hiyo ikionesha kuwa na kiwango kidogo cha muda wa watu kufanya kazi ambapo watu wanafanya kazi kati ya masaa mawili au matatu kwa siku.

Naye Godwini Martini ambaye ni mtafiti mkuu kutoka ofisi ya Waziri mkuu,amesema tafiti huo yanamuhimu kwa wizara kuyafanyia kazi maeneo yaliotajwa huku akiitaka jamii kuzidisha muda wa kufanya kazi ili kuweza kuongeza idadi ya ajira.

Kaimu Meneja wa takwimu za ajira na bei kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu, James Mbongo,akizungumza juu  Utafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2020 na 2021 kwa Kanda ya Mashariki.
Godwini Martini ambaye ni mtafiti mkuu kutoka ofisi ya Waziri mkuu, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya umuhimu wa Tafiti hiyo
Sehemu ya Madiwani na Watendaji wa Mtaa waliohudhuria  mkutano huo wasilisho la Tafiti


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...