Na Mwandishi Wetu, DODOMA
Serikali ipo katika mchakato wa kuhamishia shughuli zote za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambapo kwa sasa Shirika hilo linajihusisha na shughuli za uendeshaji na usimamizi wa Mkongo huo na shughuli nyingine zipo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye katika kikao kazi na wakandarasi wajenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kilichofanyika jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine alikabidhi vyeti vya kukamilisha ujenzi wa Mkongo wa Taifa kwa zabuni za mwaka 2020/21 kwa kampuni ya Raddy Fiber Ltd, Telecom Associate, TTCL na Huawei Tanzania.
“Kama nilivyozungumza Bungeni wakati wa wasilisho la hotuba ya Bajeti ya Wizara hii Mei 20, 2022 kuwa tupo katika mchakato wa kuhamishia shughuli zote za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Shirika letu la TTCL, Wizara imeulea mpaka umekuwa na sasa upo tayari kukabidhiwa kwa Shirika hilo”, Amezungumza Waziri Nape
Ameongeza kuwa, hana mashaka na uwezo wa Mkurugenzi wa Shirika la TTCL Mhandisi Peter Ulanga katika kusimamia shughuli zote za Mkongo na ana matumaini makubwa kuwa ataweza kubeba jukumu hilo pindi mchakato wa utakapokamilika kuukabidhi kwa Shirika hilo utakapokamilika
Aidha, katika kikao kazi hicho na wakandarasi Shirika la TTCL limekabidhiwa nyaraka zenye michoro ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano uliokamilika ambazo ni kilomita 72 kutoka Mangaka-Mtambaswala kilomita 105 za Arusha-Namanga kwa ajili ya kuliwezesha shirika kusimamia na kuendesha Mkongo huo wakati mchakato wa kuhamishia shughuli zote za Mkongo kwa Shirika hilo Ukiendelea
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye(Mb) akimkabidhi cheti na nyaraka za michoro Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga inayoonyesha jinsi na namna miundombinu ya Mkongo wa Taifa ulivyojengwa kutoka Mangaka-Mtambaswala (kilomita 72) na Arusha-Namanga (kilomita 105) ili kuliwezesha shirika kusimamia na kuendesha Mkongo huo
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akimkabidhi cheti cha cha kukamilisha ujenzi wa kilomita 72 za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kuunganisha Ofisi za Serikali zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma kwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Petter Ulanga katika kikao kazi na Wakandarasi kuhusu ujenzi wa Km 4,442 za Mkongo wa Taifa kilichofanyika leo Mei 23, jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza katika kikao na Wakandarasi kuhusu ujenzi wa Km 4,442 za Mkongo wa Taifa kilichofanyika leo Mei 23, jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akimkabidhi cheti cha mradi wa Mkongo wa Taifa uliokamilika mwaka 2021/2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Kandarasi ya Raddy Fibre Solution Ltd, Ramadhani Mlanzi katika kikao kazi na Wakandarasi kuhusu ujenzi wa Km 4,442 za Mkongo wa Taifa kilichofanyika leo Mei 23, jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (wa katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya Pamoja na Wakandarasi wa Mkongo wa Taifa uliokamilika mwaka 2021/2022 mara baada ya Waziri Nape kuzungumza na Wakandarasi hao kwenye kikao kazi na Wakandarasi kuhusu ujenzi wa Km 4,442 za Mkongo wa Taifa kilichofanyika leo Mei 23, jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...