Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka amewaonya madiwani wote wa chama hicho kuacha tabia ya kubweteka.
Akizungumza na wanachama wa ccm kwenye ofisi ya ccm mkoa wa Lindi, Shaka amesema baadhi ya madiwani wamesahau wajibu wao.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwaeleza madiwani wote wa ccm nchi nzima kujua wajibu wao… baadhi wanapokwenda huko kwenye mabaraza na halmashauri wanajisahu na kuweka maslahi yao mbele,nataka kuwaambia Chama kina wafuatilia kujua uwajibikaji wao” aling’aka Shaka.
Kauli hiyo ya Shaka ilikuja baada ya malalamiko kutoka kwa mmoja wa wanachama wa ccm kwenye mkutano huo Diwani wa Eneo lao ameshindwa kutimiza wajibu wake.
Shaka ambaye ameanza ziara ya siku tatu mkoani Lindi kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, Amekuwa na tabia ya kusikiliza zaidi kero kutoka kwa wananchi na kuzitolea majibu kupitia kwa viongozi wahusika.
Katika hatua nyingine Shaka amekiri kuwa kumekuwa na ombwe la viongozi wenye sifa ndani ya Chama na kwamba hatua kadhaa muhimu zimeanza kuchukuliwa.
Hiyo ni baada ya Mzee mmoja mwana ccm Bakari Omar Bakari kueleza kwamba kuna tatizo la baadhi ya viongozi wa chama hicho kupungukiwa na sifa za kiuongozi na Chama kinachukua hatua gani.
“ Nikiri kweli kuna ombwe lakini tayari hatua zimeshachukuliwa na kuanzia hivi sasa viongozi hawa wanaochaguliwa watapatiwa mafunzo ili wawe na uwezo na elimu ya kutosha” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...