Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Sheikh mkuu mkoa wa Pwani ,Hamis Mtupa amewataka Watanzania wakati wakiombea Taifa waombee na mataifa mengine yaliyoingia kwenye machafuko, Vita ili kurejesha amani kwani tofauti za mataifa hayo yanasababisha kushuka kiuchumi na mfumuko wa bei.
Aidha ameitaka jamii kusimamia maadili na kudumisha tamaduni za kitanzania kwa vijana,bila kuendekeza masuala ya utandawazi.
Akizungumza katika sikukuu ya Eid ,Mwanalugali Mjini Kibaha Mtupa alisema ,machafuko ya baadhi ya mataifa yaliyoingia kwenye migogoro ikiwemo Ukraine na Urusi yanapaswa kuombewa kila mmoja kwa Imani yake ili uchumi usidorore.
"Kuna baadhi ya watu wanamtupia lawama Rais Samia Suluhu Hassan, yeye anahusika na Nini,Mfumuko wa Bei za mafuta na bidhaa nyingine inatokana na baadhi ya mataifa kuingia katika migongano ambapo itaisha endapo yatakaa meza moja kuyamaliza ama kupatanishwa ,"Hili Ni suala la kuliombea na hakuna wakutupiwa lawama";!
Vilevile Mtupa alisisitiza maadili mema kwa watoto na vijana na kuwaasa waache Kujiingiza katika vishawishi vya kuvuta madawa ya kulevya na kukaa vijiwe bila kazi maalum.
Pamoja na hayo aliomba wananchi kujitokeza katika Zoezi la sensa agost mwaka huu kwa Ajili ya mipango ya maendeleo.
Mwenyekiti wa akinamama wakiislam Masjid quba Mwanalugali ,Mariam Mfinanga alitaka jamii ishirikiane kukemea vitendo viovu kwa watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...