Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAKAZI
wa vijiji katika Kata ya Talawanda ,Jimbo la Chalinze wilaya ya
Bagamoyo Pwani, wametakiwa kujikita katika upandaji wa miche ya
mikorosho,na kulima kisasa ili kujiwekea hazina ya siku za baadae.
Ramadhani
Biga Diwani wa Kata hiyo alitoa ushauri huo kwenye uzinduzi wa upandaji
wa zao hilo, limefanyika Kijiji cha Magulumatali, ambapo alisema zao la
korosho ni la kibiashara .
Aidha
walikagua mashamba yaliyopandwa kisasa akiambatana na viongozi kutoka
Halmashauri chini ya Seth Mgonja aliyemwakilisha Ofisa Kilimo, Raphael
Kajale ,Ofisa Ushirika na viongozi wengine, Biga alisema kuwa Serikali
imeliwekea mkakati zao hilo kwa manufaa ya wakulima wa korosho.
Aliwataka
maofisa Kilimo halmashauri kuwa karibu na wakulima, kwa kuwapatia
maelekezo sahihi yatakayowasaidia wananchi kunufaika na Kilimo hicho.
"Leo
tangu asubuhi tulifanya zoezi la kutembelea mashamba yaliyoandaliwa
kisasa na yenye mikorosho bora kiukweli yanaoendeza sana, niwaombe
wana-Talawanda tuelekeze nguvu zetu katika kupanda mikorosho, tuipulizie
sanjali na kuifanyia palizi," alisema Biga.
Kwa
upande wake Zikatimu aliishukuru Serikali kwa kuwakopesha pembejeo
sanjali na mabomba ya kupulizia dawa, na kwamba watakapovuna korosho zao
watapeleka katika ghala lililopo kijiji cha Magulumatali, ambalo
limejengwa na Serikali.
"Kitendo
cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Mama Samia kuwakumbuka
wakulima kwa kuwakopesha pembejeo na mabomba, inaonesha dhahili ni
namna gani inavyowajali wakulimai, tutakapovuna tutazipeleka katika
ghala letu," alisema Zikatimu.
Nae
Mgonja alisema kuwa hatua ya Serikali kuwapatia pembejeo na mabomba ya
kupulizia inalenga kuongeza ubora wa korosho utaoongeza kipato, huku
akiwataka wananchi hao kutokutorosha korosho na kwamba wataobainika
watakumbana na mkono wa sheria.
"Hapa
tuko na Ofisa Mtendaji na Polisi Kata, hawa viongozi wapo kwa ajili ya
ulinzi wetu, lakini niwasihi wananchi tusitoroshe korosho zetu kwa
kuwauzia kangomba, atayebainika atakumbana na mkono wa sheria," alisema
Mgonja.
Kajale aliwataka
wanaTalawanda kujiunga na chama cha Ushirika kata huku akiwaelezea
sehemu ya faida inayopatikana katika ushirika huo ni pamoja na kunufaika
na fursa mbalimbali zinazotoka serikalini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...