Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MABINGWA watetezi wa Michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) Simba SC rasmi wamevuliwa ubingwa wa Michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa Nusu Fainali uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Bao pekee la Yanga SC limefungwa na Kiungo Mshambuliaji wa timu hiyo, Feisal Salum (Feitoto) kwenye dakika ya 25 ya mchezo baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 za lango la Simba SC na kumshinda Mlinda lango wa timu hiyo, Beno David Kakolanya.

Katika mchezo huo ambao Yanga SC walikuwa bora katika dakika zote 90 walitawala mchezo na kuifanya Simba SC kuhangaika kusaka bao la kusawazisha kwenye mchezo huo wa Nusu Fainali.

Yanga SC wanafuzu Fainali ya Michuano hiyo ya ASFC wakati wakiwangoja kati ya Azam FC au Coastal Union FC ya Tanga ambao watacheza Nusu Fainali ya pili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, Mei 29, 2022.

Mshindi kati ya Azam FC na Coastal Union atacheza na Yanga SC katika mchezo wa Fainali utakaopigwa kwenye dimba hilo hilo la Sheikh Amri Abeid mapema mwezi Julai.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...