Na.Khadija Seif, Michuzi TV


BENDI tano za muziki wa dansi zinatarajia kuonesha uwezo wake jukwaa moja katika tamasha la 'Usiku wa Wafia Dansi'.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika Mei 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Gwambina, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam  Mratibu wa Tamasha hilo, Bernard James kutoka kampuni ya Cheza Kidansi Entertainment ambao ndio wadhamini amesema lengo la tamasha hilo ni kurudisha upya muziki huo.

Amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Chama cha Muziki wa dansi Tanzania (CHAMUDATA) kuhakikisha vinapaswa kutoa kipaumbile katika bendi za muziki wa dansi ili kufika mbali.

"Muziki huu una idadi kubwa ya mashabiki hivyo wajibu kuendelezwa ili vizazi vijavyo viweze kufahamu nyimbo zenye ujumbe nzuri na maadili ya nchi yetu, " James.

Mratibu huyo ametaja bendi hizo ambazo ni Msondo Ngoma Music Band, Bogoss Music chini ya Nyoshi el Sadaat na Mapacha Music Band ya Jose Mara ambazo zote zinatokea Dar es Salaam.

Aidha, kutakuwa na bendi mbili kutoka nje ya Dar es Salaam - Waluguru Original ya Morogoro na Mjengoni Classic ya Arusha.

Mwimbaji wa bendi ya Mapacha Music Band, Jose Mara amesema amejipanga vizuri kutoa burudani nzuri kwa mashabiki zake na wadau wa muziki huo.

Sanjari na  siku hiyo atazindua nyimbo zake mpya ziitwazo ' Nitakuwa Sawa' na 'Hukumu ya Mapenzi'.

Afisa Uhusiano wa kampuni ya Mo Green International ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, Kessa Mwambeleko alitoa wito kwa wadau wa muziki huo kujitokeza kwa wingi kusapoti muziki wa dansi ili kurudi kama hapo awali.

Alisema nyimbo za muziki dansi zinafanya vema na kutoa ujumbe kwa jamii kutokana na tungo zilizopo katika ngoma hizo.

Pia alieleza lengo la kudhamini tamasha hilo ni kuwapa nafasi hata wakulima kujipa nafasi ya kupata burudani ya Muziki wa dansi.

Mratibu wa Tamasha la "wafia dansi" Bernard James akizungumza na Waandishi Wahabari akitambulisha ujio wa Msimu mwingine wa tamasha hilo "linalotarajiwa kufanyika mei 28 katika ukumbi wa gwambina lounge jijini Dar es likijumuisha bendi 5 ikiwemo Msondo ngoma, waluguru original ,Mjengoni classic,Mapacha music band na Bongos Music.
Mwanamuziki Jose Mara akiongeza kuwa wanajipanga vizuri kutoa burudani Kwa Mashabiki wa Muziki wa dansi nchini katika tamasha la "wafia dansi" linalotarajiwa kufanyika mei 28 katika ukumbi wa gwambina lounge jijini Dar es salaam
Afisa uhusiano wa Kampuni ya Mo green international Kessa Mwambeleko ,ambao ndio wadhamini wa Tamasha la wafia dansi akieleza namna ya kuguswa kushiriki katika tamasha hilo lengo ni kukuza na kurudisha Muziki huo kwenye hadhi na heshima yake.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...