Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema itahakikisha inatoa kila aina ya ushirikiano kwa wabunifu waliopo nchini katika kuwawezesha kutangaza bunifu zao ndani nan je ya Tanzania.
Aidha Wizara hiyo imesema inataka kuona kunakuwa na wabunifu wengi zaidi ambao wanaibuliwa nchini kila siku na kwamba wabunifu wasikubali kuwa kimya badala yake wajitokeze na kwenda kutambuliwa na mamlaka husika.
Hayo yamesemwa na Balozi Mindi Kasiga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya serikali kwa Umma Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa akizungumza kwenye Wiki ya Ubunifu Tanzania inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Wiki hiyo imeandaliwa na Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknelojia kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi ya Teknolojia(COSTECH) pamoja na UNDP kupitia Programu yake ya Funguo na Mdhamini Mkuu ni Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania.
“Niko hapa leo kwa ajili ya shughuli hii ya Wiki ya Ubunifu Tanzania inayoratibiwa na Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania.Kitu muhimu tulichojifunza kutokana na mazungumzo tuliyoyafanya kuhusu wabunifu wa kitanzania.
“Kuna mambo ambayo yamejitokeza katika mazingira ya sasa hususani kwenye utali ambao ni muhimu sana kuhusisha ubunifu.Hatuwezi kuendelea kutangaza utalii kwa njia zile zile za zamani ndio maana hivi sasa tunaona Rais wa Samia Saluhu Hassan akiendelea kufanya promosheni ya filamu ya Royal Tour.
“Filamu inayoelezea vivutio vya utalii Tanzania kama nchi ya kipekee katika eneo la utalii,”amesema Balozi Kasiga.
Aidha wadau wa ubunifu wamejadili kwa kina nini kifanyike kwenye ubunifu kwa njia mbadala ya kutangaza na kuvutia watanzania kwenda kwenye utalii wa Tanzania.
“Kwa hiyo tulikuwa na mjadala tunaposema kutangaza utalii tunaanza na sisi wenyewe?Tunaanzaje au wanaanza Wazungu? tukaona yote yanahitajika na yote ni muhimu,”amesema Balozi Kasiga alipoelezea ubunifu katika kutangaza utalii.
Pia wameangalia ni jinsi gani wanaweza kutumia teknolojia na ubunifu kama njia mojawapo ya kuleta maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kumuelezea Mtanzania Idd John ambaye amekuja na ubunifu wa jukwaa la Safari Wallet.com.
“Jukwaa hilo unaweza kuingiza fedha kutoka kwenye simu yako ya kiganjani na ukaenda kutalii sehemu yoyote Tanzania .Kwa kutumia Safari Wallet.com unaweza kulipa fedha na kwenda kutalii kokote hapa nchini.
“Hivyo ni wajibu wetu Wizara pamoja na wadau wengine kumsaidia Idd aliyebuni Safari Wallet.com, sisi kwa nafasi yetu tunasema tutampa kila aina ya ushirikiano na ndio wajibu wetu kumsadia kila Mtanzania, tuko tayari kutumia balozi zetu kutangaza jukwaa hilo,”amesema.
Balozi Kasiga amesema Wizara hiyo ni kiungo kiunganishi kati ya Tanzania na nchi za nje ambako kuna wawakilishi na mataifa mengine nayo yanawawakilishi nchini.
Kwa upande mwingine, mtoa mada katika majadiliano yaliyohusisha wabunifu na masuala ya kikodi Donald Nsanyiwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kodi Kampuni ya KPMG amesema moja ya jambo la msingi linalopaswa kuzingatiwa ni kufahamu masuala ya kodi.
“Tumewaeleza wabunifu wakiwemo wanaojihusisha na ujasiriamali wanapoona watu wa TRA wanakuja kwenye biashara zao wasione kama wanawasumbuliwa.Hivyo tumetoa elimu ya kujua umuhimu wa kodi.”
Balozi Mindi Kasiga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya serikali kwa Umma akizungumza na waandishi wa habari kwenye Wiki ya Ubunifu Tanzania inayoendelea Ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali ambazo zinazochukuliwa na Wizara hiyo katika kushirikiana na wabunifu kutangaza bunifu zao.Wiki ya Ubunifu Tanzania imeratibuwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH pamoja na UNDP kupitia Programu yake ya Fungua.Kilele cha wiki hiyo kinatarajia kufanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kodi kutoka Kampuni ya KPMG Donald Nsanyiwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa mada iliyokuwa ikielezea umuhimu wa wabunifu wakuwemo wajasiriamali na wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kutambua masuala yanayohusu ulipaji kodi.
Mwanzilishi Mwenza wa Jukwaa la kimtandao la Safari Wallet.Com Idd John akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akielezea ubunifu wake katika kutengeneza mtandao huo.
Mmoja ya washiriki la kongamano la wabunifu akiuliza swali kwa mtalaamu wa masuala ya kodi(hayupo pichani).
Mtendaji Mkuu wa Barron Shoes Jacqueline Kawishe(kulia) akielezea ubunifu ambao amekuwa akiitumia kutengeneza viatu vya ngozi vikiwemo viatu vya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari ambapo amesema malengo yake ni kuwa na kampuni kubwa ya kutengeza viatu hapa nchini Tanzania.
Mmoja ya washirki akifafanua jambo wakati wa kongamano la wabunifu ambalo lilikuwa likijadili masuala yanayohusu umuhimu wa wabunifu kutambua masuala yanayohusu kodi.
Mmoja ya Vijana wakitanzania ambaye ameshiriki kwenye Wiki ya Ubunifu Tanzania inayoendelea Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam akielezea shughuli ambazo amekuwa akizifanya kupitia kampuni anayofanyia shughuli zake zinazotuokana na masuala ya kibunifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...