Na WAF TABORA.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametoa wito kwa wananchi kuachana
na mila na desturi potofu kuhusu hedhi na kusisitiza juu ya upatikanaji
wa huduma na vifaa vya kujihifadhi hasa taulo za kike sehemu zote kwa
makundi yote kwa bei nafuu katika jamii.
Prof.
Makubi amesema hayo leo Mei 27, 2022 wakati akitoa tamko la maadhimisho
ya siku ya hedhi salama Duniani akiwa Mkoa wa Tabora.
Amesema,
bado jamii ina uelewa mdogo kuhusu suala la hedhi, na kusisitiza
ushirikiano katika mapambano dhidi ya mila na desturi potofu kuhusu
suala la hedhi, huku akiweka wazi kuwa, hedhi salama ni afya na ni
baraka za uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
"Bado
jamii yetu ina uelewa mdogo kuhusu suala la hedhi hivyo nitoe wito kwa
jamii kuachana na mila na desturi potofu kuhakikisha upatikanaji wa
huduma na vifaa vya kujihifadhi hasa taulo za kike sehemu zote kwa
makundi yote na hata kuwa na bei elekezi katika bidhaa hii." Amesema
Prof. Makubi.
Sambamba
na hilo Prof. Makubi amesema, Wizara kwa kushirikiana na wadau
inaendelea kutoa elimu na uhamasishaji kwa jamii na shuleni ili kuongeza
ufahamu juu ya masuala ya Hedhi Salama.
Aidha,
Prof. Makubi amewashukuru wadau mbalimbali kupitia mtandao/Jukwaa la
Wadau wa Hedhi Salama (Menstrual Health and Hygiene Coalition - MHH) kwa
mchango mkubwa wanaoutoa kuhakikisha suala la Hedhi Salama linatiliwa
mkazo pamoja na kupewa kipaumbele.
Mbali
na hayo ameweka wazi kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea
kutoa elimu ya Hedhi Salama kwa jamii kwa lengo la kuhamasisha, kuvunja
ukimya na kuachana na mila na desturi potofu kuhusu hedhi na kuhakikisha
Sera ya Afya inaliweka jambo la hedhi salama kuwa moja ya vipaumbele
ili kutunza heshima na utu wa mwanamke.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...