Na. WAF - Kigoma
Maadhimisho
ya Hedhi Salama Duniani yametoa fursa ya upimaji afya wa Magonjwa
mbalimbali pamoja na utoaji wa elimu juu ya Afya unaendele katika
viwanja vya Mwanga Community Center uliopo mkoani Kigoma.
Maadhimisho
hayo yameanza rasmi Mei 24, 2022 katika viwanja hivyo yanaenda sambamba
na utoaji wa huduma za upimaji wa Magonjwa na utoaji wa elimu na
kutarajiwa kumalizika kwa kilele Mei 28, 2022.
Maadhimisho
hayo ya kilele yatahudhuriwa na wananchi pamoja viongozi mbalimbali wa
Wizara ya Afya ambapo mgeni rasmi atakuwa Mke wa Makamu wa Rais wa
Tanzania Mama Mbonimpae Mpango.
Miongoni
mwa huduma za upimaji wa magonjwa zinazotolewa hapo ni pamoja na
upimaji wa Saratani ya mlango wa kizazi, UVIKO-19,UKIMWI, shinikizo la
damu (Presha), upimaji wa Sukari pamoja na uzito na huduma hizo zote
zinatolewa bure.
Aidha, elimu pia inatolewa juu ya Uzazi wa mpango, namna nzuri ya ulaji wa vyakula (lishe)na ukweli kuhusu Covid-19.
Hivyo,
wakazi wote na wananchi wa Mkoa Kigoma wanakaribishwa kujitokeza kwa
wingi kwenda kupata huduma zote za upimaji pamoja na elimu zinazotolewa
katika viwanja hivyo Bure.
Hata
hivyo Maadhimisho hayo siku ya kilele May 28, 2022 yatasindikizwa na
mbio za km 5, zitakazo anzia katika viwanja vya Mwanga community center
kuanzia saa 1:00 asubuhi zikiongozwa na viongozi kutoka wizara ya Afya,
wanafunzi pamoja na wananchi.
Maadhimisho
hayo ya Hedhi Salama Duniani, kitaifa yanafanyika Mkoani Kigoma katika
viwanja vya Mwanga Community Center yenye kauli mbiu isemayo "HEDHI NI
TUNU NA MSINGI WA AFYA, DHAMIRIA KUWEKEZA KATIKA NYANJA ZOTE."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...