NA MWANDISHI WETU
Naibu katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amekemea tabia ya wachukua taarifa wasio waadilifu wanaochukua taarifa za kijiografia  (GPS) za sehemu moja kutolea taarifa kwenye eneo jingine. Jambo hilo linaharibu kazi data na linasababisha mfumo kutoa taarifa zisizosahihi.
“Watendaji mkagaue na kujiridhisha kuhusu taarifa za kijiografia (GPS), hasa pale inapotokea taarifa hizo kufanana eneo moja na jingine allisema Naibu Katibu Mkuu Mmuya.”
Hayo yamesemwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa operesheni ya anwani za makazi katika wilaya ya Kilwa na Rufiji. lazima tukusanye taarifa za kijiografia kwa kila nyumba ambayo inaenda kutambuliwa kwa sababu taarifa hizo za kijografia  zinatofautiana.
ninawapongeza wananchi wa Kilwa na Rufiji kwa uelewa na muitikio wao katika kutekeleza Operesheni ya anwani za makazi, na umuhimu wake kwa Sensa ya watu na makazi. Tuendelee kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa operesheni ya anwani za makazi.
“Ninatoa wito kwa wananchi wote, kujiwekea namba ya kudumu kwenye mageti au milango ni jukumu lao alisema Naibu Katibu Mkuu Mmuya.”
Akihitimisha Injinia wa Tarura Agatha Mtwangambate amesema kwa awamu ya kwanza  idadi ya vibao vya barabara ni kwa ajili ya barabara zote zilizosajiliwa, na vitawekwa katika mwanzo wa barabara na mwisho wa barabara. Kadri operesheni ya anuani za makazi inavyoendelea tutaanza kuzitambua barabara mpya na kuziwekea vibao.Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rufiji Mhe. Juma Ligomba Na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rufiji Bwn. John Kayombo mbele ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Rufiji wakati akikagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi wilaya hiyo.Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya (katikati) akitembea katika Mtaa wa Mkwanyule kukagua utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa.Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza jambo na Mtendaji wa Kijiji cha Umwe Kaskazini kata ya Umwe Bwn. Emmanuel John katika kukagua utekelezaji Operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Rufiji.Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya akizungumza na wananchi katika barabara ya Matumbi kukagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...