Na.Khadija Seif, Michuzi TV

Mabondia Wanaocheza Uzito Wa Super Feather Kg 60 Jackson Malinyingi na Said Mkola Wamesaini Mikataba  Kwa ajili Ya Kupanda Ulingoni Kutoana jasho  katika Pambano la raundi 8 Kwenye "Usiku Wa Kisasi" Linalotarajiwa Kufanyika Juni 25 Mwaka Jijini Dar es salaam.

Wakizungumza Mara Baada ya Kusaini mikataba hiyo Mabondia hao Kila mmoja akijinasibu Kuibuka na Ushindi dhidi ya Mpinzani Wake.

Huku Bondia Omary mpemba na Ally Kilongora kutoka Ngumi Kunasia Gym,
wamesema wamejipanga kikamilifu kuelekea siku ya pambano na wamewataka wapinzani wao kujiandaa kisaikolojia kwa ajili ya kupokea kichapo cha paka mwizi.

Nao makocha wa Mabondia hao Kocha Max Mawe na Man Pakiyao wamesema,Tayari wamewafua vya kutosha mabondia wao na wamewataka wapinzani kutokujihusisha na imani za kishirikina badala yake waoneshe Mchezo mzuri utakao pendwa na mashabiki Wa Ngumi.

Bondia Said Mkola (Upande wa Kushoto) na Bondia Jackson Malinyingi (Upande wa kulia)mara Baada ya Kusaini Mkataba kwa ajili ya Kupanda ulingoni june 25 katika pambano la usiku wa Kisasi litakalopigwa Jijini Dar es salaam.

Bondia Said Mkola  akisaini Mkataba kwa ajili ya Kupanda ulingoni june 25 katika pambano la usiku wa Kisasi litakalopigwa Jijini Dar es salaam.
Jackson Malinyingi (Upande wa kulia) akisaini Mkataba hii leo Kwa ajili Ya Kupanda ulingoni june 25 katika pambano la usiku wa Kisasi litakalopigwa Jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...