Cde. Michael Msuya Katibu wa UVCCM (M) Dar es Salaam ametoa wito huo kwa Vijana wa Dar es Salaam wa kumsaidia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutoa Elimu na kupeleka uelewa kwa watanzania juu ya mambo Mbalimbali yanayoendelea nchini.

Cde. Msuya ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na Wanahabari baada ya Zoezi la usafi wa kiwanja cha CCM Biafra Kinondoni ambapo CCM inakwenda kufanya uwekezaji Mkubwa.

Cde. Msuya alisisitiza huku akitole Mfano wa Changamoto ya Ongezeko la Bei ya Mafuta ya vyombo vya usafiri kwa kuwaomba vijana kuelezea chanzo cha Changamoto ambapo alisema ni lazima Watanzania wajue Changamoto iliyoko katika nchi zinazozalisha mafuta kwa maana ya OPEC na Zile OPEC Plus kuwa kipindi cha UVIKO 19 Bei ya Mafuta Ghafi iliporomoka sana na kupelekea nchi hizo kupunguza uzalishaji wa Mafuta.

 Akaeleza kuwa kwa sasa Mjadala ni kuziomba nchi za Falme za Kiarabu na Saudi Arabia kuongeza uzalishaji wa mafuta jambo ambalo linautata kwa Nchi hizo wenyewe kudai hazipokei Maelekezo kutoka nchi za Mangaribi hivyo wataamua wao wenyewe bila kushawishiwa, Cde. Msuya akaeleza Changamoto ya Urusi juu ya Vikwazo vya uchumi na ukizingatia ni miongoni mwa nchi wazalishaji wakubwa wa Nishati ya Mafuta jambo linalopelekea pia uhaba wa mafuta na kupanda bei kwa bidhaa hiyo katika soko la dunia.

Hivyo Cde. Msuya anasisitiza ipo haja ya wananchi kuelezwa chanzo cha Tatizo wajue na sio kubeza Serikali na Jitihada kubwa zinazofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

“Ni lazima Vijana tutoke tumsaidie Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza mambo haya na mengine mengi kwa kina ili kuleta uelewa wa pamoja katika jamii na Sisi Vijana wa DSM Tunaendelea Kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hadsan kwa Kazi Nzuri anayoendelea kuifanya” Alisisitiza Cde. Msuya

Sambamba na hilo Cde Msuya hakuacha Kuongelea Swala la Usalama katika mkoa wa DSM ambapo aliwaomba vijana kuendela kutoa Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuwapatia taarifa mbalimbali zinatakazo fanikisha kutokomeza Vitendo vya Panya Road katika Jiji la Dar es Salaam. 


Mwisho Cde. Msuya akatoa Wito kwa Vijana Kujitokeza siku ya Royal Tour kwa mko wa Dar es Salaam ili kusikia Matunda ya Royal Tour kwa Taifa

.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...