Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAFANYAKAZI sita wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha nia ya kutokuendelea na kesi dhidi yao.

Washtakiwa walioachiwa huru ambao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 58.3 kwa kujilipa posh ni, Charys Ugullum, Raymond Wigenge, Ezekiel Mubito, Adelard Mtenga na Abdallah Juma.

Mapema, wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Hassan Dunia amedai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo kuwa kesi hiyo leo Mei 17, 2021 ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini DPP amewasilisha maombi ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Kufuatia taarifa Bach hiyo Hakimu Tarimo alikubaliana na ombi la upande wa mashtaka kwa kufuta kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5 ya 2018 na kuwaachia huru washitakiwa hao.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kati ya Mei na Desemba 2016 katika Ofisi za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA wakati huo) kwa sawa TMDA washtakiwa waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 58,390,000 fedha ambazo ni posho za wafanyakazi waliokuwa wamesaini malipo yao jambo lililosababisha kujilipa mara mbili.

Katika kesi hiyo, shahidi mmoja pekee ndiye aliyekuwa ametoa ushahidi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...