NA FARIDA SAID, MOROGORO.

Walimu wametakiwa kutumia stadi za maisha katika kuwasaidia wananfunzi wanaorudi shule kupitia mfumo rasmi (reentry) baada ya kusitisha masomo yao kwa muda kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito kwa watoto wa kike ili waweze kupata elimu na kutimiza ndoto zao.

Hayo yameelezwa  mkoani Morogoro na   Mkurugenzi wa uthibiti bora wa shule kutoka Wizara ya Elimu Bi. Euphrasie Buchuma wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa walimu kutoka katika Halmashauri tatu za Chemba, Malinyi na Manispaa ya Morogoro.

Alisema kupitia stadi za maisha kutawasaidia walimu kufundisha wanafunzi wengi zaidi kutimiza ndoto zao za kielimu kwani wananfunzi watakuwa wanafahamu namna bora ya kuishi kutokana na mazingira waliopo.

Pia amewahakikishia walimu kuwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI inatambua mchango wa walimu katika kuleta mapinduzi makubwa ya elimu hapa nchini hivyo itahakikisha elimua ya stadi za maisha inawafikia vijana wengi zaidi kupitia walimu wa unasihi na ushauri nasaha.

Kwa upande wake Mkurugrnzi wa miradi kutoka CAMFED TANZANIA Bi.Nasikiwa Duke alisema mafunzo hayo ya siku tatu yanalenga kuwaongezea maalifa walimu wa stadi za maisha, unasihi na ushauri ili waweze kuwajenga vyema wanafunzi wao  wakiwemo  wale walioacha shule na kurudi katika mfumo rasmi ( reentry ).

Alisema matarajio yao baada ya mafunzo hayo ni walimu kuja na mpango mkakati wa uwasilishaji wa mafunzo hayo kwa walimu wengine katika shule walizotoka na jinsi gani wanaenda kuimarisha huduma ya unasihi, ushauri, stadi za maisha na malezi kwa wananfunzi wa shule za sekondari.

“CAMFED pamoja na Wizara ya Elimu tuliona ni vyema kutoa mafunzo haya kwa walimu ili yaweze kuwasaidia katika mfumo huu wa reentry ambao ulipitishwa na  Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan mwaka jana ambao unawawezesha wanafunzi walioacha shule kurudi kuendelea na masomo yao katika mfumo rasmi.”alisema Bi. Duke.

 Mafunzo hayo yameratibiwa  na Wizara ya Elimu, TAMISEMI pamoja na CAMFED yamelenga kutoa elimu kwa walimu therathini (30) wa shule za sekondari wa stadi za maisha, unasihi na ushauri kutoka Halmashauri tatu za Malinyi,Chemba na Manispaa ya  Morogoro.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...