Na Mwamvua Mwinyi, MAFIA

Mkuu wa mkoa wa Pwani , Abubakari Kunenge ametoa Rai kwa wananchi waliovamia  na kuweka  kambi  za uvuvi katika kisiwa cha NYORORO ,wilaya ya MAFIA kutii agizo la serikali kuhama mara moja katika kisiwa hicho .

Rai hiyo imekuja kutokana na kisiwa hicho kuwa ni eneo tengefu kwa ajili ya mazalia ya samaki katika bahari ya Hindi na sio vinginevyo.

Kunenge alitoa rai hiyo wakati alipofanya ziara ya Kikazi katika kisiwa hicho kukutana na wananchi hao ambao wamevamia kisiwa hicho ambacho  hakina huduma za kijamii na kuanzisha makambi ya kudumu.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, serikali kupitia  kwa  Waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki  tayari imeshakutana na  wananchi  na kuagiza waondoke katika eneo hilo.

"Lakini bado wameendelea kuwepo wanakaidi  jambo ambalo limemlazimisha katibu mkuu wa wizara hiyo kutoa maelekezo mengine kwa uongozi wa mkoa akiutaka uongozi huo usimamie  agizo la kuondolewa kwa watu hao";!

Amewataka wananchi hao kuheshimu  agizo hilo kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na hakuna mtu yoyote aliyeko juu ya sheria,

Vilevile aliwaasa, wananchi hao kupitia kwa mwenyekiti  SAIDI LIKUWA kuunda  kamati ya watu watano  wafike ofisini kwake ili kujadiliana namna ambavyo wataweza kumaliza tatizo hilo kwakuwa serikali ya awamu ya sita  inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassani ni sikivu na ina wajali wananchi wake.

Kwa upande baadhi ya wakazi hao wameiomba serilali kuhalalisha kisiwa hicho kuwa makazi ya watu na kuanzisha kitongopji ndani ya kisiwa hicho ili wananchi waweze kupata huduma za kijamii .
 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...