Na.Khadija Seif,Michuzi TV
Akizungumza
hayo wakati wa kukabidhi zawadi Kwa washindi wa Shindano la Uni talent
,Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka (BASATA) Agustino Makame amesema
wanafunzi vyuoni wanatakiwa kuzikimbilia fursa kikamilifu hususani
Mashindano ya kusaka vipaji Ili kuendeleza vipaji vyao pamoja na kukuza
tasnia ya burudani nchini.
"uwepo
wa Mashindano ya kusaka vipaji ikiwemo ya "Uni talent" ni ishara tosha
kuwa wanafunzi vyuoni Wana uwanda mpana wa kuonyesha vipaji vyao na
kuendeleza vipaji hivyo kutokana na wengi wao kuendelea kupeperusha
vyema bendera ya burudani hivyo ni muhimu kwao kuzikimbilia fursa hizo."
Hata
hivyo Afisa huyo ametoa wito Kwa wadau na Makampuni kuunga Mkono vipaji
vyuoni na BASATA kushirikiana na Kampuni iliyoandaa Shindano hilo ya
Maroon entertainment kuwa bega Kwa bega kuhakikisha Msimu ujao unakua wa
kitofauti zaidi.
Mkurugenzi
wa Kampuni iliyoandaa Shindano la "Uni talent" Chrispine Kiondosha
amesema hatimae wanahitimisha Msimu wa 3 na kuhakikisha washindi
wanakabidhiwa zawadi zao.
Pia
ameeleza kuwa Shindano hilo litakua endelevu ili kuhakikisha
wanaendeleza vipaji Kwa wanafunzi vyuoni na msimu wa 4 unakua msimu
mzuri.
Aidha katika
makabidhiano hayo mshindi wa kwanza ni kutoka Chuo cha Sanaa Cha
Bagamoyo (TaSUBa), "African cousins" wakiondoka hundi ya shilingi
milioni 10 pamoja na nafasi ya kusoma nje ya nchi, Mshindi wa pili "Afro
dreams" wamekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 5 na nafasi ya tatu
ikishililiwa na Osmond Soka akikabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi
milioni 1.
Mkurugenzi wa Maroon entertainment Chrispine Kiondosha,
ambae pia ndio Mratibu wa Shindano la "Uni talent" akizungumza na
waandishi Wahabari Jijini Dar es salaam mara baada ya kukabidhi zawadi
Kwa washindi watatu katika Shindano hilo.
Mshindi wa tatu Osmond Soka katika akisikiliza kwa makini namna mchakato ulivofanyika Hadi kupatikana Kwa washindi wa Shindano la "Uni talent"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...