Na. Edmund Salaho/MKOMAZI.
Watumishi
52 wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wamehitimu mafunzo
ya mabadiliko ya utendaji kazi kutoka mfumo wa kiraia kwenda mfumo wa
kijeshi yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi yakiwa na lengo la
kuwajengea uwezo watumishi hao kufanya kazi katika mfumo wa jeshi la
uhifadhi.
Awali,
akisoma taarifa ya mafunzo hayo, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na
Maendeleo ya Biashara-TANAPA, Herman Batiho alisema mafunzo hayo
yalihusisha askari wa Uhifadhi 50 na maafisa Uhifadhi wawili
lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi na kuimarisha usimamizi wa rasilimali zilizopo katika maeneo ya hifadhi.
Akifunga
mafunzo hayo, Kamishna wa Uhifadhi-TANAPA, William Mwakilema amewataka
watumishi hao kutekeleza kwa vitendo mbinu na maarifa waliyoyapata
kwenye mafunzo hayo kwa maslahi ya taifa.
“Ni
tegemeo langu kwamba mafunzo haya yamewajengea uzalendo, uadilifu,
ujasiri , utayari, kujiamini, na ari kubwa katika kulinda rasilimali za
taifa. Niwapongeze sana mmeonyesha kwa vitendo na mkatekeleze kwa
vitendo yote mliyojifunza.” alisema Mwakilema.
Kamishna
Mwakilema amewatahadharisha “Silaha ni chombo ambacho kinatakiwa
kitumike kwenye shughuli za ulinzi na matumizi yake yawe sahihi. Silaha
zitumike pale tu unapokabiliwa na tukio ambalo linaweza kuhatarisha au
kupoteza maisha yako.”
Aidha,
Kamishna Mwakilema alipongeza juhudi kubwa zilizofanywa na wakufunzi
wa mafunzo hayo katika kuwajengea uwezo wahitimu hao kusimamia na
kulinda Rasilimali za Wanyamapori
na Misitu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...