Na.Vero Ignatus,Arusha

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassimu Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dr.John Pima, pamoja na watumishi wengine watano kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya mali za umma

Akitoa taarifa hiyo katika ukumbi wa Kimataifa wa mkutano AICC Arusha leo tar 24/5/2022 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Jiji hilo, alimuagiza Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kufanya uchunguzi mara moja, pamoja na kusimama ,kwa kamati zote kutoka Tamisemi zilizokuwa zikifanya uchunguzi awali, zisimame na kurudi makao makuu

Aidha Waliosimamishwa ni pamoja na Mariam Shaban Mshana (mwekahazina)Innocent Maduhu (Mchumi) Nuru Sakware,Alex Daniel MKIWA ambapo Mhe. Waziri Mkuu aliwaambia wakiwa salama watarudi kazini ikiwa siyo basi.

Mhe.Majaliwa amesema Mkurugenzi alimwagiza mweka hazina Mariam shabani mshana kulipa mil 103 kwenye akaunti binafsi ya Innocent Maduhu ,akaagiza tena mil 65 kwenye akaunti binafsi no 43301602080 ya Alex Daniel siku ya tar 14/4 na usingizie ni masulufu ya kuweka vifusi kwani yeye ni injinia?ukaagiza tena kuweka pesa kwenye akaunti binafsi no 40808002463 Nuru Kinana mil 65,ambapo tarehe hizo mbili 14 na 28 alitoa idhini mil 233 za halmashauri ya jiji na fedha hizo hazikutumika kwa malengo ya serikali bali kwa malengo binafsi

''Halafu sasa mnashirika katika kughushi nyaraka mbalimbali Efd mashine na anawadai kwasababu yeye anadaiwa na TRA nyie hamna hela mil 300 mlishazitumia tar 28 mnafanya mchezo na eletonic inaibua kila kit una ilieleza kila kituna wewe mkurugenzi ndiyo unaagiza hayo mambo,mmehamisha watumishi 45 kutoka January,idara ya utawala mmehamisha 2,idara ya fedha 26 Elimu sekondari 2msidingi 2 tehama 1 mipango 1,ujenzi 1,maendeleo ya jamii 1 mkahamisha na watumishi wawili vibarua halima msangi mkampeleka hai,Betty kirungwa Monduli ameshindwa kwenda''alisema Mhe.Majaliwa.


Mhe.Majaliwa alihoji juu ya uhamisho wa watu 5 kati ya mwezi wa 4 na wa 5 ambao ni John Selemeni Mtango,(Longido)Marchus shindika(Mipango amehamishiwa meru)Sela Bina (utumishiamehamisiwa Kibiti) Richard Gerald elimu msigi amehamishiwa Musoma,Mbwana Msangi mwekahazina amepelekwa Hai, kijumlisha 45na hawa 5 jumla 50,utumishi gani huo mlikuwa na mkakati gani alihoji mhe.Mjaliwa.mmehamisha hao mmeletawatu wenu waje kusshughuklikia mradi

''Takukuru fuatilia hayo hii ni fedha ambazo Raisi wetu anajitahidi kuzitafuta usiku na mchana watu wanarahisisha mambo na kufanya mambo unawekeana kwenye akaunti binafsi yao binafsi ni utaratibu wawapi?alihoji Mhe.Waziri Mkuu''.

Amesema kuwa Serikali imeweka mfumo mzuri wa fedha,ambapo amesema hawawezi kufanya mzaha na nchi ambayo inatakiwa kubadilika, madiwani wanatamani kuona maendeleo ya fedha zinazoletwa na mhe.Rais lakini bado wapo watumishi ambao hawasikii wanafanya ubadhirifu

‘’Nyie hamkujua ya kwamba hata benki kuu unaweza ukaipata hii documenti ya malipo unayofanya kila siku na kujua mmempa nani ,mkuu wa idara unakwenda kununua vifusi jambo ambalo hata katibu kata angeliweza kwenda kununua huo ni utarati u wawapi,tuliwaambia mpige bati geji 28 nyie mkapiga 30 nyingine mkapeleka nyumbani’’ Yule Joel w akule Longido arudi hapa alihamishwa hapa ili asije kusema hayohatuwezi kukubaliana nayo.

Mhe.Majaliwa amesema serikali haiwezi kufanya mzaha na Jiji kama La Arusha ambalo linahitaji kubadilishwa ,ambapo Rais ameweka dhamira ya kulibadilisha

Awali Waziri Mkuu ambaye alikuwa mkoani Arusha kwa ziara ya siku moja na kukagua masoko ya Mbauda, Kilombero na Machame alibaini kuwa mabati yaliyotumika kwenye ujenzi wa vibanda vya wamachinga ni ya geji 30 wakati kanuni zinataka majengo yote ya Serikali yatumie mabati ya geji 28.


Mkazi wa Mbauda, Bi Mary Mushi ambaye ni mfanyabiashara ya nyanya katika soko hilo, alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanachangishwa sh. 500 ili kununua dizeli ya kuendesha jenereta linalotumika kutoa umeme sokoni hapo. Umeme huo unawashwa hadi saa 3.30 usiku.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alipomtaka Meneja wa TANESCO wa wilaya, Bw. Amiri Chambua aseme ni lini wataweka umeme, Bw. Chambua aliahidi kukamilisha kazi hiyo kesho (Jumatano, Mei 25, 2022). Alikiri kupokea barua ya maombi tangu mwezi uliopita na kudai kwamba walikuwa kwenye mchakato wa maandalizi.

Kuhusu kadhaa ya askari mgambo, Waziri Mkuu amewataka watumie weledi na maarifa kwenye kazi yao ya ulinzi. “Mtu kama anauza eneo lililoruhusiwa, askari tumieni miongozo na waeleweshwe; na pia zile mali mlizoweka kule Depot warudishieni kwa sababu mitaji ni midogo,” alisema na kuamsha shangwe miongoni mwa wafanyabiashara hao.
Waziri mkuu Kassim Mjaliwa akifanya ukaguzi katika moja ya soko jijini Arusha mapema leo

Waziri mkuu Kassim Mjaliwa akizungumza nawananchi mara baada ya kufanya ukaguzi wa badhi ya masoko Jijini Arusha mapema leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...