Na Shamimu Nyaki- WUSM, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu leo Mei 10, 2022 jijini Dodoma amekutana na wataalamu wa Ala za Muziki wakiongozwa na Mwalimu Mstaafu wa Shule za Sekondari Alexander Ngonyani ambao wanapitia Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo na Wimbo wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika wakati wa uimbaji na hatimaye kuyarekebisha ili nyimbo hizo ziimbwe kwa usahihi.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Yakubu amesema kuwa Wimbo wa Taifa ni miongoni mwa Tunu za Taifa, hivyo unapaswa kuheshimiwa.

"Nawasisitiza kubainisha makosa yaliyopo kwenye nyimbo hizo, pamoja na usahihi unaotakiwa ili sisi kama Serikali tuchukue hatua ikiwemo kutoa elimu Kwa jamii ili makosa hayo yasirudiwe"Amesema Bw.Yakubu.

Kwa upande wake Mzee Ngonyani amesema kuwa chimbuko la kazi hiyo ni kutokana na kubaini makosa mengi katika uimbaji wa nyimbo hizo unaofanywa na Taasisi, Shule na katika hafla mbalimbali za kitaifa, na tayari ameshawasiliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na BASATA ambao wamepokea utafiti huo ambao na kushauri aonane na uongozi wa Wizara ili kufanyiwa kazi ipasavyo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu akizungumza na na wataalamu wa Ala za Muziki ambao wanapitia Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo na Wimbo wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika wakati wa uimbaji na hatimaye  kuyarekebisha ili nyimbo hizo ziimbwe kwa usahihi leo Mei 10, 2022 jijini Dodoma.


Mwalimu Mstaafu wa Shule za Sekondari Alexander Ngonyani ambae ni mtaalamu wa Muziki akizungumza wakati alipokutana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu leo jijini Dodoma ambapo wanapitia Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo na Wimbo wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika wakati wa uimbaji na hatimaye  kuyarekebisha ili nyimbo hizo ziimbwe kwa usahihi.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...