TAASISI ya Binti Shupavu imetoa elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Msasani ‘A’ iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo ulioambatana na utoaji wa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Khadija Seif ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Michuzi Media amesema kuwa lengo lao ni kuona mabinti wanakuwa shupavu na kupinga vishawishi ambavyo vitawafanya kutotimiza ndoto zao.

“Kwanini Binti Shupavu, lengo ni kuona mabinti wanakuwa shupavu na kusimama wenyewe na kupinga vishawishi, tunaangalia wasichana ambao wanapata vishawishi na kukatiza ndoto zao,” amesema Hadija na kuongeza kwamba,

“Tupo tayari kukemea hivyo vishawishi na kuwaambia mviepuke ili mfikie ndoto zenu,”.

Amewataka wanafunzi hao kuwa huru kumweleza mzazi/mlezi wa kiume wanapokuwa katika kipindi cha hedhi ili waweze kupata huduma stahiki ikiwemo kununuliwa taulo za kike.

“Na unatakiw akujenga urafiki na ndugu zako wa damu, kama vile baba, mama, mjomba, bibi, shangazi na sio watu wengine wakiwemo bodaboda ambao watakuingiza katika vishawishi hatarishi,” amesema Khadija.

Kwa upande wake Mwanamasumbwi wa Tanzania Selemani Kidunda akizungumza kwa niaba ya akina baba, amesema kwamba Binti Shupavu ni yule ambaye anajiamini na mwenye uwezo wa kuepuka vishawishi hatarishi.

Aidha amewataka watoto wa kike kutambua kwamba hedhi sio ugonjwa na kwamba wanapokuwa katika kipindi cha hedhi wasiogope kuwaambiwa wazazi wao yaani baba na mama.

“Baba ni kama mama usiogope kumwambia, ukipata tatizo mshirikishe ili akusaidie,” amesema Kidunda.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Msasani wilayani Kinondoni Mkoani Dar es Salaam, Kichiki Njovu amewataka watoto wakike wanapokuwa na tatitizo wasiwaeleze watu wa barabarani na badala yake wawaambie wazazi au waalimu kwa msaada zaidi.

“Usimwombe msaada mtu yeyote barabarani mfano bodadoda kwani hata kupa msaada bure. Mwisho wake utapata ujauzito na kushindwa kutimiza ndoto zako kwani hedhi ni chanzo cha kupata ujauzito,”.

“Kwahiyo sasa hivi ukikutana na mwanaume utapata ujauzito, ukipata ujauzito nani atakutunza, unakuta wazazi wengine ni wakali wanakufukuza,”.

Hivyo amewataka watoto hao wakike wajitunze kwamba wasikimbilie kupata mimba za utotoni

Bondia wa Ngumi za kulipwa Selemani Kidunda akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi la kilele cha siku ya Hedhi salama kwa wasichana wa shule ya Msingi Msasani A kwa watoto wenye ulemavu ambapo zoezi hilo liliandaliwa na Taasisi ya binti shupavu .


Mwenyekiti wa Taasisi ya binti shupavu Khadija Seif akiwa ameambatana na Bondia wa Ngumi za kulipwa Selemani kidunda katika zoezi la ugawaji wa taulo zakike kwa wasichana wa shule ya Msingi Msasani A Jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...