
Baadhi ya wakulima na wafugaji katika vijiji vya idui, ndembo na utengule Kata ya Utengule katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wamevamia maeneo ya pori tengefu ndani ya bonde la kilombero na kuweka makazi ya kudumu, kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji hivyo kutishia hifadhi ya bonde hilo pamoja na shughuli za uwekezaji ikiwemo vitalu vya uwindaji wa kitalii.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni na watafiti kutoka chuo kikiu cha Dar es salaam uliainisha hatari ya uharibifu wa mazingira katika bonde hilo kutokana na shughuli za kibinadamu, ambapo mkuu wa kitengo cha doria wa kampuni ya KILOMBERO NORTH SAFARI ambao ni miongoni mwa wawekezaji wa vitalu vya uwindaji, akakiri kuwepo kwa hali mbaya ya uvamizi katika maeneo hayo.
Kwa upande wao wananchi wanaodaiwa kuvamia hifadhi hiyo walisema wanaishi katika maeneo hayo kihalali baada ya kupewa na uongozi wa kijiji tangu muda mrefu, ambapo mhifadhi toka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini TAWA, Lawrence Okode, ambaye pia ndiye Kamanda wa pori la akiba la Kilombero alisema mkakati uliopo kwa sasa ni kuhifadhi uoto wa asili wa hifdhi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hanji Godigodi, nae alikilri uvamizi huo na kudai wanachosubiri ni utekelezaji wa maamuzi ya timu ya mawaziri nane waliokwishatembelea embelea bonde la Kilombero nakujionea uharibifu huo na mgogoro uliopo..
Licha ya sifa ya bonde hilo kuwa na ardhi oevu, mito mingi inayoingia, pori la akiba na shughuli za uwindaji wa kitalii, maji ya bonde hilo yanategemewa kwa asilimia kubwa katika uzalishaji wa umeme bwawa katika mradi mkubwa wa Julius Nyerere unaoendelea kujengwa Rufiji mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...