Na Amiri Kilagalila
Mwenyekiti
wa Chama Cha madereva wa IT (ITDA) wanaoendesha magari kutoka bandarini
na kuyasafirisha kwenda nchi mbalimbali bwana Adam Mwenda ameishukuru
mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kutambua thamani ya
madereva wanaotoa huduma hiyo ndani bandari baada ya mamlaka hiyo
kuwapatia eneo litakalotumika kuwa sehemu rasmi ya kupumzikia madereva
hao.
Akizungumza na
waandishi wa habari akiwa kwenye ofisi za chama hicho zilizopo jengo la
Maktaba ghorofa ya tatu jijini Dar es Salaam amesema, Aprili 29, mwaka
huu wakati wa kikao kilichokuwakutanisha madereva wa ITDA na kamanda wa
kikosi cha usalama barabarani nchini, SACP Wilbroad Mutafungwa
kilichofanyika bandarini walitoa ombi kwa TPA juu ya eneo la kupumzika
na kujihifadhi katika eneo namba mbili ndani ya bandari hiyo.
Aidha
kufuatia ombi hilo hatimaye TPA imekubali kutoa eneo hilo na sasa
ujenzi unaendelea wa kujenga viti na meza kwa kutumia saruji pamoja na
kujenga bafu na choo vitakavyotumiwa na madereva hao.
“Hivi
sasa ujenzi unaendelea, mafundi wameshajenga viti na meza vya zege
pamoja na choo, kwa hiyo tunakwenda kutengeneza mradi mkubwa na heshima
kubwa kwa madereva wote, kwa hiyo ni wakati mzuri kusema kwamba ITDA
tunaweza kufanya mambo kwa ushirikiano na kushirikiana na taasisi zote
za serikali na kuendelea kuaminika zaidi,” alisema Mwenda.
Mwenyekiti
huyo ameishukuru TPA kwa kutoa eneo hilo na kueleza kuwa uamuzi huo
hivi sasa unaleta imani kubwa kwao na kwamba sasa madereva wa ITDA
wameanza kuonekana ni wathamani kubwa katika kusukuma gurudumu la
maendeleo hapa nchini na ndiyo maana mamlaka hiyo imeamua kutoa eneo
hilo.
“Nawaomba madereva kuwa wastaarabu wanapokwenda kwenye maeneo yale tukapumzike tukiwa na amani kabisa na tukiamini lile ni eneo letu sahihi kwa mapumziko yetu na pia kukaa pale bila kubughudhiwa,niwaombe wale wateja wanaokwenda kushoto na kulia tuwaeleze
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...