Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) komredi Daniel Chongolo, ameendelea
kutoa msisitizo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kushughulikia Tembo
Wavamizi wa mazao ya Wananchi mkoani Simiyu.
Ametoa
kauli hiyo leo June 02, 2022 wakati alipowasili katika Wilaya Itilima
mkoani Simiyu ukiwa ni muendelezo wa ziara yake yenye lengo la kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 katika mikoa ya Shinyanga
na Simiyu.
Akizungumza
katika kata ya Nkoma, komredi Chongolo amesema Wizara ya maliasili na
Utalii ni lazima ihakikishe inaleta Suluhu ya kudumu kukomesha
Changamoto ya Uvamizi wa Tembo kwenye Mashamba na Makazi ya Wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...