Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amemtaka mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga kuwawezesha wakulima wa Jimbo Hilo kuhakikisha Kila tarafa wanapata Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti Ili kuongeza thamani ya zao hilo ambapo kwa Mkoa wa Simiyu, Itilima inaongoza kwa uzalishaji wa alizeti.
"Najua
Mbunge wenu ana wajibu wa kuwasaidia mashine za kuchuja mafuta ya
alizeti, wasaidie wananchi Hawa wapate mashine za kuchuja mafuta ya
alizeti angalau kwa mashine moja kwa Kila tarafa na hili litawasaidia
sana kuongeza thamani ya zao hili."
Katibu Mkuu
ameongeza kuwa kitendo Cha kufunga mashine, wakulima wataanza kuuza
mafuta badala ya kuuza alizeti zenyewe, ambapo kwa sasa mafuta ya
alizeti ndio mafuta bora na ghali zaidi, hivyo wananchi watapata fedha
za kutosha tofauti na sasa.
Chongolo ameyasema
hayo leo tarehe 2 Juni, 2022 alipowasili Wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu
wakati akiendelea na ziara yake yenye lengo la kukahamasisha uhai wa
Chama ngazi za mashina na Kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...