Na Mwandishi wetu- Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu  ameongoza kikao cha tisa cha kamati hiyo.

Kikao hicho kimefanyika Juni 02, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali , Wakurugenzi wa Taasisi na wataalamu ambapo wamejadili hatua zilizofikiwa kuhakikisha zoezi la uwekaji wa anwani katika makazi linakamilika kama lilivyokusudiwa.

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia TAMISEMI Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmmuya, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba na Mratibu Anwani za Makazi Zanzibar Bw. Abdalla Dai Abdalla.

Aidha Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni muendelezo wa  maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 Agosti  2022 nchini  ambayo  hufanyika  kila baada ya miaka 10.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) (katikati) akiongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi  kilichofanyika Juni 02, 2022 ukumbi wa ofisi hiyo Jijini Dodoma, (kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya na wa (kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza.


Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akieleza jambo katika kikao hicho.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...