Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewataka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wanapoendelea na shughuli ya kusambaza maji kwa kujenga matenki na kuchimba visima, wajenge matenki makubwa yatakayokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji mengi kutoka ziwa Victoria.
Lengo la kufanya hivyo ni kuiepusha serikali hasara nyingine ya ujenzi wa matenki kwani mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria unaendelea na wilaya ya Itilima upo katika mpango huo.
Akizungumza kwenye ziara yake akiwa Itilima Chongolo ametoa mwito kwa RUWASA matenki ambayo yatakuwa na uwezo wa kubadilika, baadaye watakapokamilisha mradi wa maji ya Ziwa Viktoria. Maji yatakuja mengi, hivyo badala ya kutumia visima sasa yaunganishwe matenki hayo na mfumo wa maji ziwa Viktoria badala ya kuanza kujenga mapya.
Chongolo amesema sasa hivi RUWASA ni lazima wajiandae kuwa tayari kupokea maji yatakapofika kutoka ziwa viktoria, kwa kuwa Serikali imedhamiria Wana Itilima kupata maji kutoka Ziwa Viktoria,
"Hapa Itilima ni lazima maji ya Ziwa Vitktoria yafike, na Sio hapa tu yatafika Bariadi na Meatu, ambapo Maswa, Kishapu, Shinyanga mjini Kahama na maeneo mengine maji tayari yamefika, na hii ndio kazi ambayo anaifanya Mhe. Rais Samia kwa wananchi wote nchini." amesema.
Akiwa katika katika Mkutano wa shina namba 7 kata ya Lagangabilili, baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu Wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila kuwa Mkoa huo umepokea shilingi Bilioni 23 kwa ajili ya kujenga matenki ya maji na kuchimba visima ambapo baada ya taarifa hiyo ametoa ushauri huo kwa RUWASA.
.jpeg)
.jpeg)

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Itilima mkoani Simiyu Mhe.Njalu Silanga wakati akikagua mradi wa maji wa Nyamalapa akiwa kwenye ziara yake mkoani Simiyu Leo.
.jpeg)
Wananchi waliofika kwenye mradi huo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Ndugu David Kafulila wakati akifafanua jambo mara baada ya kukagua mradi wa maji wa Nyamalapa akiwa kwenye ziara yake mkoani Simiyu Leo. Kulia ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Itilima Mhandisi Hussein Yahya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...