Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
BONDIA wa Ngumi za kulipwa katika uzani wa (Bantam kg 53) Hamidu kwata anatarajia kupanda ulingoni kwa mara nyingine tena dhidi ya Bingwa wa PST Ally Ngwando kwenye Pambano kuu la "Usiku wa kisasi" juni 25 uwanja wa taifa wa Ndani Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Michuzi TV, Muandaaji wa Pambano hilo Meja Selemani Semunyu amesema maandalizi yanaendelea vizuri kwa sasa na mabondia wameweka kambi wakiendelea na mazoezi yakujiweka sawa kuelekea pambano hilo .
"Maandalizi yanaendelea vizuri mabondia wako kambini wanafanya mazoezi Ili kuhakikisha katika mapambano yao wanafanya vizuri huku ingizo jipya Msanii kutoka Twangapepeta Khalid chokoraa akijipanga kumchakaza mpinzani wake usiku wa kisasi ".
Hata hivyo Semunyu amesema mpaka sasa pambano hilo la "Usiku wa kisasi" limekua na muitikio mzuri kutokana na damu nyingi changa kujitokeza kutaka kushiriki na kuonyesha uwezo wao katika mchezo huo wa masumbwi hasa vijana wengi kutokea mtaani licha ya ingizo hilo jipya la Khalid chokoraa likiwa pambano linalosubiriwa kwa hamu zaidi na mapema Juni 18 mabondia wote wanatarajiwa kupima uzito.
Pambano la Ally Ngwando pamoja na Hamidu kwata ni miongoni mwa pambano linalosubiriwa Kwa hamu sana kwani ni pambano la marudio baada ya mapambano yao matatu kutoka sare hivyo usiku wa kisasi mashabiki wanasubiri kujua nani bingwa.
Mabondia hao ambao watacheza pambano kuu linalotarajiwa kuwa na mshike mshike wanarudia kwa mara ya tatu baada ya mapambano yao ya awali kutoka sare na hivyo kuacha kisasi cha kutaka kujua nani Mbabe zaidi ya mwenzake.
Hamidu kwata ambaye amekita kambi huko Mbezi Louis DSM katika mazoezi ya kufa na kupona amesema hivi sasa anakuja na zawadi ya ushindi wa KO kwa Watanzania na wadau wa masumbwi.
Hata hiyo Mwalimu wa bondia huyo Walles Danford a.k.a Coyo Mawe amesema Ally Ngwando amekua akipatiwa mabondia wenye viwango vidogo jambo ambalo limepeleka kushinda kujua kiwango cha Kwata na kuchagua kupambana naye juni 25.
"Ally ngwando hadi sasa anamiliki mkanda wa ubingwa wa Taifa wa PST baada ya kumtwanga James Kibazange kwenye pambano la Champion wa kitaa lililofanyika machi 20,2022 Indoor Taifa."
Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Hamidu Kwata akizungumza machache kuelekea pambano la "usiku wa kisasi" linalotarajiwa kufanyika Juni 25 katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo kwata atapanda uringo dhidi ya mpinzani wake Ally Ngwando
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...