Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , amesema kuwepo idadi kubwa ya walimu miongoni mwa watumishi wa umma Zanzibar itumike kuwa mtaji muhimu wa kusaidia kuleta mageuzi makubwa yenye tija katika sekta ya elimu na kuchangia kasi ya maendeleo ya taifa.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko Skuli ya Sekondari ya Fiderl- castro Vitongoji Mkoa wa Kusini Pemba alipozungumza na Maafisa wa Elimu na walimu wakuu wa Skuli mbali mbali za Kisiwani Pemba akiwa katika mfululizo wa ziara yake ya kutembelea sekta ya elimu nchini.
Amesema walimu ni wadau muhimu wanaolazimika kushiriki kikamilifu katika azma ya serikali ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu yanayoahitajika nchini yatakayosaidia Zanzibar kupigia hatua na kwenda sambamba na maendeleo ya elimu yanavyokwenda duniani.
Amesema kwamba mageuzi yanayohitajika ni yale yatakayoisaidia Zanzibar kuishi katika ulimwengu na maendeleo ya elimu duniani kuepuka kuwa wasindikizaji wa maendeleo yanavyokwenda katika nchi mbali mbali duniani.
Aidha Mhe. Othmana amasema kwamba mageuzi makubwa yatakayofanywa itaifanya Zanzibar kurejesha heshima kubwa ya elimu katika ramani ya dunia na kuweza kushindana kimaendeleo nan chi zilizoweza kupiga hatua kubwa kama zile Singapore na kwengineko duniani.
Amesema kwamba kwa kuzingatia haja ya maendeleo ni lazima Zanzibar kama zilivyo nchi nyengine duniani kufanya uwekezaji na mageuzi makubwa stahiki katika elimu kwenye maeno mbali kama zilivyofanya nchi nyengine zilizoweza kupiga hatua.
Aidha amesema kwamba katika jitihada za kuleta mageuzi kwenye sekta hiyo ni lazima pia kuwepo ushiriki mpana wa sekta binafsi ili kuchangia kasi ya maendeleo hasa kwa kuzingatia kwamba changamoto zilizopo katika sekta hiyo ikilinganishwa na uchumi wa Zanzibar ni mzigo mkubwa kwa serikali unaohitaji ushiriki wa kila mdau kukabiliana nao.
Amewataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa ari na kujitolera huku serikali ikifanya mabadiliko makubwa ya maslahi ya walimu ikiwemo mishahara yao inayotarajiwa kulipwa mwezi Julai mwaka huu.
Naye Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mhammed Mussa amesema kwamba serikali inaendelea na utekelezaji wa azma yake ya kubporesha maslahi ya walimu kuanzia julai mwaka huu na kuwataka walimu pamoja na mambo mengine kuwa na juhudi na kufundisha nidhamu kwa vijana mbali mbali nchini.
Mhe. Lelala amsema kwamba serikali kwa sasa pia inatoa kipaumbele cha ushirikishwaji wa wa sekta binafasi katika jitihada za kuimarisha sekta ya elimu nchini katika hatua mbali mbali.
Kwa upande wao walimu mbali mbali walieleza kwamba Sekta hiyo imekabiliwa na changamoto mbali mbali yakiwemo maslahi duni, uhaba wa vitendea kazi pamoja na upungufu mkubwa wa walimu hasa katika masmo ya sayansi jambo linalopunguza ufanisi na maendeleo katika sekta hiyo.
Kwa upande wao wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) tawi la Bjenjamin Mkapa Pemba wameulalamikia uongozi wa chuo hicho kwamba wamekuwa wakikosa huduma ya umeme mara kadha kwa Zaidi ya wiki moja baada ya kumalizika umeme ulionunuliwa jambo ambalo linadhoofisha juhudi zao za kutafuta elimu.
Katika ziara hiyo Mhe. Makamu leo ametembelea Chuo cha Kiislamu Micheweni, Skuli ya binafasi ya Ambasha iliyopo Shengejuu, Chuo Kikuu cha taifa SUZA tawi la Benjamin Mkapa Mchangamdogo na baadae kuzungumza na maafisa wa elimu pamoja na walimu wakuu wa skuli za mikoa miwili ya Pemba huko Skuli ya Fedel Castro Vitongoji.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...