Mkurugenzi wa Kampuni wa JKRBS International Dk.Riziki Seleman Nkya akiwa katika picha tofauti tofauti akiwa ameshika baadhi ya dawa zinazovyotengenezwa kwa miti shamba

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya JKBRS International ambayo ni bora na namba moja kwa kutoa huduma za kitabibu kwa kutumia miti shamba kutibu magonjwa sugu na ya kawaida imewaomba wananchi wataofika Maonesho ya Sabasaba kufika kwenye banda lao.

JKBRS International  kwenye maonesho ya Sabasaba mwaka huu wapo katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, hivyo wananchi ambao watafika kwenye banda hilo wafike kwao kupata huduma za kitabibu.

Akizungumza leo akiwa kwenye maandalizi ya kujiandaa na Maonesho ya Sabasaba, Mkurugenzi wa JKBRS International Dk.Riziki Seleman Nkya amesema ofisi zao ziko Ubungo Plaza na kwa kipindi hiki timu zima ya madaktari wao watakuwa Sabasaba kuwahudumia wananchi.

“Tutakuwa hapa na timu nzima ya madaktari wetu ili kuhakikisha kila mteja wetu anayekuja kwa ajili ya kupata huduma za matibabu anahudumiwa.Wataofika Sabasaba  tunawaomba wasikose kufika banda hili la Wizara ya Maliasili na sisi tuko kwenye banda hili.

“Njooni mjipatie huduma zenu, mjipatie matibabu.Najua wengi mlikuwa mnajiuliza mtatupata wapi katika Maonesho haya ya Sabasaba, hivyo  tunawaambia tuko hapa Banda la Maliasili na Utalii na maandalizi yote yamekamilika.”

Dk.Riziki Seleman Nkya amesema afya yako ni mtaji wako, hivyo wanaosumbuka na magonjwa sugu  na magonjwa ya kawaida, maralia sugu, UTI, waliokosa watoto , matatizo ya meno na uvimbe katika kizazi , sambamba na magonjwa mbalimbali watahudumiwa na kupona.


“Katika banda hili la Maliasili na Utalii ukiingia ndani kama unakwenda kuangalia wanyama basi sisi tuko mwanzoni kabisa,”amesema na kuongeza kampuni yao nibora kabisa na ndio kampuni ya kwanza ya tiba asili nchini

Amefafanua wengi huenda  wakijiuliza kwanini wako Sabasaba au kwanini wanatumia  maonesho hayo huduma za kitabibu, jibu  ni kuwa wanajua watu wengi wanashindwwa kufika kwenye hospitali zetu au kliniki zao zilizoko sehemu mbalimbali, hivyo wanaamini kwenye maonesho hayo watu wengi wakienda na itakuwa rahisi kufika kwao.

“JKBRS tumesajiliwa na Serikali  tumeamua ni lazima tuwepo Sabasaba tukiamini watu wengi wanakuja katika maonesho haya lakini tunafahamu kila mtu anahitaji kinga, anahitaji tiba.

“Unajua kutumia dawa sio lazima uumwe , kuna dawa nyingine unatumia kama kinga na tunasema kinga yako ndio afya yako, ni lazima ujikinge, ni lazima utumie dawa kama unaumwa na ili upate tiba sahihi basi ni tiba inayotokana na miti shamba.

“Ni dawa zilizoanza kutumika enzi na enzi kabla ya Adam na Hawa basi tuliwekewa bustani ile ya Edeni, tukapatiwa miti ambayo ni sahihi na usitumie dawa ilimradi dawa , bali tumia dawa iliyothibitishwa.

“JKRBS tumekuwa tukifanya tafiti kwa ajili ya kukupatia tiba na kinga iliyosahihi. Njoo tukuhudumie na mawasiliano yetu ni 0753185592 au 0744111115.”

Kwa upande wake Dk.Alex Huale amesema wataendelea kuwa hapo Sabasaba na kubwa zaidi ni kama vile nembo yao inavyojitambulisha.

  

“JKBRS International tumefanikiwa kuishika dunia kutokana na uwezo tulionao katika kutibu magonjwa sugu na hapa ndio suluhisho lake, tunayo dawa inayojulikana kwa jina la Life.Njoo tukurejeshee tabasamu lako kwa kutatua changamoto za kiafya unazokabiliana nazo.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...