Serikali mkoani Mtwara imetekeleza maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi yaliyotolewa na Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka kuhusu kuharakishwa kwa usambazwaji na ugawaji wa pembejeo kwa wakulima wa korosho ambao ulilalamikiwa na wananchi wakati wa ziara yake mkoani humo ya uimarishaji wa chama na ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali mkoani humo ni kuwa pembejeo hizo zimeanza kusambazwa na magari katika maghala ya vyama vya msingi kwa ajili ya kutolewa kwa wakulima wa korosho.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti alitoa ahadi kwa Ndg Shaka kuwa ndani ya saa 24 badala ya siku saba alizotoa pembejeo zitaanza kuwafikia wakulima.

Wananchi wamekishukuru na kukipongeza Chama Cha Mapinduzi kufanikiwa kusukuma uharikishwaji wa pembejeo hizo ambazo serikali ya CCM awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imezitoa bure kwa wakulima ili kuongeza tija na faida kwa kilimo wanachokifanya.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...