
Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa akikabidhiana mkataba na Mwenyekiti wa migahawa ya Samaki Samaki, Carlos Mella (Kalito) wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Vodacom na migahawa hiyo itakayotoa zawadi kwa wateja wa Vodacom watakaolipia kwa kutumia M-Pesa watarudishiwa asilimia 10 ya malipo yao na pia wateja wote watapata huduma ya bure ya WiFi.

Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa akizungmza wakati hafla ya kusaini mkataba wa kampuni ya Vodacom na migahawa ya Samaki Samaki ya jijini Dar es Salaam, wateja wa Vodacom watakaolipa kwa kutumia M-Pesa watarudishiwa asilimia 10 ya malipo yao na pia wateja wote watapata huduma ya bure ya WiFi.
KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini imesaini mkataba na Mwenyekiti wa migahawa ya Samaki Samaki ya jijini Dar es Salaam
hafla hiyo ya kusaini mkataba imefanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 3,2022.
Amesema kuwa Wateja watakaopata huduma katika migahawa hiyo Vodacom itatoa zawadi kwa wateja watakaolipia kwa kutumia M-Pesa watarudishiwa asilimia 10 ya malipo yao na pia wateja wote watapata huduma ya bure ya WiFi.
Ubia huo mpya unalenga kuwawezesha na kuwazawadia watumiaji wa Vodacom wanaotembelea migahawa ya Samaki Samaki na kutumia mfumo wa Vodacom wa M-Pesa Kufanya malipo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa alisema, “Tunafurahia sana kushirikiana na Samaki Samaki, jina ambalo limejizolea wapenzi wakweli miongoni mwa wateja wake., kama vile ilivyo kwetu sisi Vodacom Tanzania. Kwa hiyo ni vema kabisa kwetu sisi kushirikiana kuwapatia wateja wetu huduma bora na kuwazawadia uamiinfu wao kwetu.”
Samaki Samaki walianza na tawi moja tu mjini Dar es Salaam ambalo liliwapatia umaarufu haraka na kupelekea kuanzishwa kwa tawi lao la pili huko Masaki. Migahawa hiyo hutoa vyakula safi vya baharini, katika mandhari bora zaidi na kuwapatia wateja huduma bora mgahawani kwa bei nafuu.
Kwa ushirikiano huu mpya, unaolenga kuwahusisha zaidi vijana, watumiaji wa Vodacom wanaotembelea Samaki Samaki wataweza kutumia mtandao wa kasi ya juu wa Vodacom 4G kupitia Wi-Fi bila malipo kwenye migahawa hiyo. Zaidi ya hayo, wale wanaolipa kupitia M-Pesa watarejeshewa 10% ya pesa taslimu kwenye vyakula na vinywaji vyao.
Vodacom inatumia fursa hii kuendeleza kampeni ya kutumia malipo ya kidijitali kwa matumizi ya kila siku. Malipo ya kidijitali ni salama kwa wafanyabiashara kwani wanalinda mtaji kutokana na hatari za wizi au upoteajina vile vile humuondolea mlipaji adha ya kutafuta ATM, kupanga foleni kwenye benki, kutafuta chenji au kubeba pesa taslimu itakayohitajika kwa miamala yake.
Kwa wageni wanaotembelea migahawa hiyo siku za Jumamosi, kutakuwa na matukio mbalimbali ya uhamasishaji ili kuzalisha ushirikiano na kutakuwa na shughuli nyingi za kusisimua na za kuburudisha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Samaki Samaki, Carlos Mella alisema, “Ushirikiano huu umekuja wakati muafaka, kwa kuwa tumejenga wateja waaminifu wanaofurahia huduma zetu kuu na tunajua tukiwa na mfumo wa M-Pesa, tutaweza kupunguza adha za malipo kwa wateja wetu wakiwa kwetu. Pia tunatazamia shughuli nyingi tulizopanga kwa watumiaji wa Vodacom kwenye migahawa yetu. Nyote mtafurahi!.”
Ushirikiano huu mpya unaendana na mkakati wa Vodacom Tanzania wa kuongeza uelewa wa chapa na ushirikishwaji wa wateja ili kuwazawadia watumiaji wa huduma zake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...