Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
akiongoza matembezi ikiwa ni sehemu ya Bonanza la Pamoja la Benki ya
CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), yaliyoanzia kwenye viwanja vya Bunge na
kuishia kwenye Uwanja wa Jamhuri na kufuatiwa na Michezo Mbalimbali
ikiwemo ile ya Soka, Pete na Kikapu, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Picha zote na Othman Michuzi.
Akizungumza katika bonanza hilo, Spika alisema kuwa bonanza hilo limeleta msisimko na mwamko mkubwa kulinganisha na miaka ya nyuma, ambapo mwaka huu idadi ya washiriki imeongezeka na kufanya maana na lengo halisi la mashindano hayo kupata umaarufu jijini Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya CRDB inaipa kipaumbele michezo, kwani michezo ni afya, inaleta umoja na upendo, inawaleta pamoja Wafanyakazi wa Benki na wadau mbalimbali wa Michezo nchini. Hivyo Benki inatumia bonanza hilo kama sehemu tu ya kuisogeza karibu na Serikali, Bunge na wadau mbalimbali nchini ili kupata nafasi ya kusikiliza mahitaji yaliyopo na kujua namna gani benki inaweza kushiriki katika mipango ya maendeleo ya nchi na kuthibitisha kauli mbiu yake ya “Ulipo Tupo” na kuwa ni benki inayomsikiliza Mteja.
Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Ally Laay aliwashukuru Wabunge na wadau mbalimbali wa serikali na wananchi waliohudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi kushiriki bonanza hilo lililotanguliwa na matembezi yaliyo anzia katika viwanja vya bunge vikiwemo vikundi mbalimbali vya Jogging, wanafunzi wa vyuo na Sekondari pamoja na wananchi kwa kutambua umuhimu wa michezo.
Mashindano hayo yalimalizika kwa Timu za Bunge la Jamhuri wa Muungano kutwaa ushindi wa jumla kwa Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Pete pamoja na Ule wa kuvuta kama (Tag of War) katika bonanza hilo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa
tatu kushoto) akiwa sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,
Abdulmajid Nsekela pamoja na viongozi wengine wakiongoza mazoezi ya
viungo muda mfupi baada ya kumaliza matembezi 'CRDB Bank Pamoja
Bonanza', yaliyoanzia kwenye viwanja vya Bunge na kuishia kwenye Uwanja
wa Jamhuri na kufuatiwa na Michezo Mbalimbli ikiwemo ile ya Soka, Mpira
wa Pete, Kikapu nk. jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa
Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
(kulia) akifurahi pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa
Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita, wakati akipokea medali yake
baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za mita 100, katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Cosato Chumi baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Picha ya pamoja na Mabingwa wa CRDB Bank Pamoja Bonanza.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimvisha medali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
akimvisha medali, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
akimvisha medali, Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Ridhiwani Kikwete katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
akimvisha medali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
akimkabidhi medali, Nahodha wa Timu ya Bunge ya mpira wa pete, Mhe. Mama Salma Kikwete, katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson
akimvisha medali, Mhe. Mama Salma Kikwete, katika
Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza),
lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Mashindano ya kuvuta kamba kati ya Waheshimiwa Wabunge na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Mchezaji mahiri wa mpira wa pete wa timu ya Bunge, Mhe. Mama Salma Kikwete akiwaonyesha kazi timu ya Baraza la Wawakilishi, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akitafuta nafasi wakati wakiwapelekea mashambulizi wapinzani wao, wakati wa Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...