Na John Walter-Babati
MKUU wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amewaagiza viongozi wa kata,mitaa na vijiji kwa kudhibiti vitendo vya uhalifu katika maeneo yao kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Babati, Mkuu wa wilaya alisema "Hali ya ulinzi na usalama kwa sasa ni ya kuridhisha,hatuna matukio makubwa yaliyotokea yanayoashiria uvunjaji wa amani katika maeneo yetu."
Twange amesema yapo matukio yaliyokithiri ya uvunjaji wa nyumba nyakati za mchana na usiku.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amewapongeza Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Babati kwa kusimamia vizuri hali ya ulinzi na usalama katika wilaya pamoja na maeneo yake yote yanayounda wilaya hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...