Na Amiri Kilagalila, Njombe
MWENYEKITI wa Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amewataka wanawake wa mkoa huo kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kazi zote anazofanya kwa kuwa kwa sasa nchi imetulia.

Amebainisha hayo wakati akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo wilaya ya Njombe alipofanya ziara katika jimbo la Lupembe,huku akidai kuwa nchi imekuwa na amani na utulivu mkubwa na kutoa rai kwa wanawake wa jumuiya hiyo pamoja na watanzania kuendelea kuilinda amani tuliyonayo kwa kuto sababishwa na wanasia wasio kuwa na nia njema.

“Ninachofurahia ni amani,nchi imetulia yaani unaamka unajua unaenda shambani bila bughudha yeyote,lakini kuna kipindi mfanyabiashara unalala unawaza sijui kesho nitakutana na magereza au nini.Lakini sasa hivi amani nchi imetulia”alisema Scolastika Kevela

Ameongeza kuwa "Uongozi Bora,siasa safi zinazofanywa na Chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti wetu Mh.Samia Suluhu Hassan ndio zinapelekea nchi yetu kuendelea kuwa na amani"

Hata hivyo amesema Tanzania itakapochezewa,wahanga wakubwa itakuwa ni akina mama na watoto zaidi.

"Niwaase wanawake kuwa watanzania tukichezea amani,watakaoumia zaidi ni watoto,wanawake na wazee,ni muhimu sana wanawake wenzangu kuzingatia hili"Amesema Scolastika Kevela

Vile vile amebainisha kuwa Rais Samia ameendelea kufanya vizuri na kuboresha mahusiano ya ndani na kimataifa kwa kuwa nchi ya Tanzania sio kisiwa na kupelekea Mtanzania kwenda nchi yeyote.

Faraja Mbanga ni diwani wa viti maalum tarafa ya Lupembe na Christina Msolwa ni baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao chao na mwenyekiti katika shule ya msingi Kidegembye wameshukuru kwa maelekezo mbali mbali waliyopewa na viongozi wao huku wakiongeza kuwa katika jimbo lao watahakikisha uwepo wa amani wakati wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...