Na Mwandishi Wetu, Mtwara

NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM, Musa Mwakitinya, amewataka vijana wa Seneti Mkoa wa Mtwara kuendelea kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi katika maeneo yao ili kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika mahafali ya Idara  ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoani Mtwara, Mwakitinya amesema kijana ndio jeuri ya Chama, hivyo amewaomba vijana mkoani  humo kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao kwa kuhamasisha wananchi watambue umuhimu wa Sensa ya watu na Makazi nchini.

Mwakitinya amesema kwasasa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya  Rais Samia Suluhu Hassan ipo tayari kuhakikisha inasimamia kikamilifu Sensa ya watu na Makazi ili Watanzania wote wapate kuhesabiwa kikamilifu katika maeneo yao.

" Ni jukumu la kila Kiongozi kujua umuhimu wa Sensa ili mwananchi wa chini  apate elimu na sisi Kama Vijana mlisimamie ili kila Kijana asimamie ili kwa maslai ya Nchi yetu ya Tanzania.

Mwakitinya pia amewasii wale wote ambao wanaotembeza  hujuma mbaya kwa wananchi kuhusu  Sensa basi Jeshi la Polisi muliangalie ili kwa manufaa ya Nchi yetu katika Kuwapatia huduma iliyobora katika kila maeneo ya Nchi.

" Sisi Vijana tunajukumu kubwa la kuhakikisha tunasimamia Zoezi la Sensa liende vinzuri na kila mwananchi apate kuandikishwa na ajue Umuhimu wa Sensa katika Nchi yetu ." Mwakitinya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...