Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Talack ( aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao Maalum cha Baraza la Maalum la Manispaa ya Lindi.



Na Mwandishi Wetu,Lindi

MKUU wa Mkoa wa Lindi  Zainab  Telack ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( TAKUKURU) mkoani humo kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani waliohusika na ucheweshwaji wa ukamilishaji wa kazi katika mradi wa Barabara.

Barabara ambaazo zimecheleweshwa ni Uhuru,Msonabarini na mzunguko wa barabara ya Mchinga zilizojengwa Manispaa kwa kiwango cha lami .

Akizungumza leo na Baraza Maalumu la Madiwani Manispaa ya Lindi la  kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  kwa mwaka wa fedha 2021-2022 Taleck ameishauri kuimarishwa kwa udhibiti wa ndani katika kusimamia utekelezaji wa mikataba.

Telack amesema Mhandisi Mshauri hakikishe  anasimamia usimamizi wa karibu kwa  wakandarasi  ili kuweza kumaliza kazi iliyobaki katika mradi huo bila kuchelewa na kutoa huduma kwa wananchi .

Ametumia nafasi hiyo kueleza wazi waliohusika na ucheleweshwaji wa mradi huo wa Barabara uchunguzi ufanyike na kisha hatua ichukue mkondo wake ikiwa pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria ikiwemo Mahakamani.

Aidha amekemea tabia za baadhi ya wananchi kuchoma moto mashamba yao karibu na barabara na kuleta adha kwa watumiaji wa barabara na  kulitaka Jeshi la polisi kufanya doria na kuwakama  wale wote watakaochoma moto na kuwachukulia hatua za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...