NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita kufanya uchunguzi wa miradi yote ya TASAF inayotekelezwa kwenye Halmashauri zote za Wilaya za Mkoa huo.
Ndejembi ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na Waratibu wote wa TASAF kwenye Halmashauri za Wilaya katika Mkoa huo ambapo amewataka kusimamia miradi hiyo kwa weledi na uadilifu.
" Nimesikiliza maelezo ya kila mmoja wenu, haiwezekani miradi ya Serikali itofautiane gharama, Inawezekana vipi Darasa lililojengwa kwa fedha za Uviko-19 gharama yake iwe Milioni 20 halafu Darasa lililojengwa kwa fedha za TASAF liwe Sh Milioni 25 na hii miradi yote inasimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri, hili halikubaliki.
Nikuombe Mkuu wa Mkoa miradi hii yote inayotekelezwa kwenye Halmashauri za Wilaya zote za Geita, TAKUKURU waje wakague waangalie kama thamani ya fedha inaendana na miradi hii. Ripoti ya Takukuru ije mezani kwangu kabla ya Bunge la Bajeti halijaisha na mimi mwenyewe ntakuja field kuona," Amesema Ndejembi.
Naibu Waziri Ndejembi pia ameagiza Waratibu hao wa TASAF kuhudhuria vikao vya CMT kwenye Halmashauri zao ili kuhakikisha pia masuala yanayohusu TASAF yanajadiliwa.
" Tulishatoa maelekezo kila mratibu wa TASAF aingie kwenye vikao vya CMT hili siyo jambo la hiyari ni maelekezo ambayo TASAF na Tamisemi walisaini , Kila Jumatatu mnavyojadili masuala yenu ya Halmashauri ni lazima mratibu wa TASAF aingie.
Sasa Mkuu wa Idara au Mkurugenzi ambaye hataki kutekeleza maelekezo ya Serikali sisi tutamuona hatoshi na tutamchukulia hatua, hivyo nielekeze tena kila mratibu wa TASAF aingie kwenye vikao vya CMT," Amesema Ndejembi.
Ziara ya Naibu Waziri Ndejembi ilikua ya kuzungumza na Waratibu wa TASAF Mkoa wa Geita pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi 54 ya TASAF inayotekelezwa kwenye Ujenzi, Afya na Elimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...