NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ametolea ufafanuzi namna gani Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Wakuu watapimwa utendaji kazi wao kupitia mfumo ambao umewekwa na Serikali wa kupima utendaji kazi wa watumishi wake.

Ndejembi ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi aliyetaka kujua mkakati wa Serikali katika kuhakikisha watumishi wa umma wanatimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria.

" Ofisi ya Rais Utumishi tayari tumetekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuandaa mfumo wa kuwapima watumishi wetu na tayari tumekamilisha mapitio ya mfumo wa OPRAS unaotumika kupima tathimini ya mtumishi wa umma na sasa tunafanya usanifu wa mifumo mipya ambayo itaanza kufanya kazi mwaka wa fedha wa 2022/23.

Hivyo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya watapimwa na mamlaka za uteuzi wakati Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri watapimwa utendaji kazi wao na Katibu Mkuu Kiongozi," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...