NA KARAMA KENYUNKO MICHUZI TV
MAHAKAMA Kuu Masijala Kuu imesema, kesho Aprili 30, 2022 itaanza kusikiliza kesi ya msingi ambayo ni maombi ya kuomba kibali cha kufungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wabunge 19 wa viti maalimu (CHADEMA) wakiongozwa na Halima Mdee
Hatua hiyo imekuja baada ya Chadema kupitia wakili wake, Peter Kibatala kuomba kuondoa mapingamizi ya awali waliyoyaweka dhidi ya maombi hayo.
Kufuatia hayo, Jaji Mustapha Ismail ameamuru kuwa wabunge hao 19 waliovuliwa uanachama wao waendelee kubakia katika nafasi yao ya ubunge hadi pale maombi yao hayo yatakoposililizwa na kutoleaa maamuzi.
Akielezea sababu za kuondoa Mapingamizi hayo Kibatala ameeleza kuwa mapingamizi hayo yalikuwa yameambatana na kiapo kinzani ambacho nacho wameomba kiondolewe mahakamani.
"Tumeamua kuondoa mapingamizi na kiapo kinzani hapa kwa na kuzingatia kanuni zinasema kuwa maombi ya msingi yanatakiwa yasikilizwe ndani ya siku kumi na nne tangu yanapopelekwa mahakamani na kutolewa maamuzi hivyo endapo wataendelea na mapingamizi hayo yatasababisha kesi kushindwa kumalizaka kwa wakati.
Baada ya ya kibataka kueleza hayo upande wa Jamuhuri ambao wanawakilisha wajibu maombi namba mbili na tatu ambao ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiongozwa na Stanley Kalokola wamedai hawana pingamizi dhidi ya maombi hayo ya Chadema.
Ameri hiyo imetolewa na jaji Mustapha Ismail baada ya wajibu maombi wa kwanza kipitia mawakili wao wakiongizwa na Peter kibataka kuomba kuondoa mapingamizi ya awali waliyoyaweka dhidi ya maombi hayo.
Kufuatia Chadema kuondoa Mapingamizi yao, mawakili wa kina Mdee wakiongozwa na Ipilinga Panya wamedai wamepokea maombi ya kibatala na hawapingi maombi yake ya kuondoa mapingamizi ya awali na wanakubalina na sababu alizozitoa na oda ya zuio la muda iendelee wakati wakisubiri mahakama isikilize shauri la msingi namba 27 ya mwaka 2022.
Kwa mkutadha huo, awakili wa waleta maombi ambao nao walikuwa wamewasilisha kiapo kinzani cha kupinga maombi hayo naomba wameyaondoa mapingamizi yote 6 ili waendee na muda na kumaliza kesi hiyo ndani ya siku 14.
Hata hivyo Jaji Ismail ameridhia maombi ya pande zote tatu na ameruhusu Chadema kuwasilisha kiapo kinzani kesho kabla ya saa nne asubuhi ambapo kesi ya msingi itaanza kusikilizwa.
Halima na wenzake walipeka maombi hayo mahakamani hapo kuomba kibali cha mahakama kufungua kesi ya kupingwa kuviwa uanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Mdee na wenzake walivuliwa rasmi uanachama wa Chadema May 12 mwaka huu na baraza la wadhamini la chama hicho.
Mwisho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...