Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini Lewis Nzali akigimza na waandishi wa habari juu ya shughuli mbalimbali za kuhifadhi na utunzaji mazingira Mkoa wa Arusha.



Na.Vero Ignatus, Arusha

Katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na wadau wengine imeshiriki katika shughuli ya upandaji miti zaidi ya 1250 katika sehemu mbalimbali Mkoani Arusha.

Lewis Nzali ni Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini amesema suala la kupanda miti na kuitunza ni la muhimu kwa ustawi wa Mazingira ya Taifa, hivyo hatua hiyo inayokwenda sambamba na uhimili wa mabadiliko ya tabianchi lakini pia unawezesha mazingira ya Miji kuwa ya kijani na mandhari nzuri ya kuvutia.

" Baraza kwa kushirikiana na wadau tumeshirikinkatika upandaji miti katika mtaa wa Engavunet kata ya mkonoo, miti 250 ilipandwa katika shule ya msingi na sekondari Mkonoo, Halmashauri ya Meru zaidi ya miti 500 kandokando ya mto, nduruma na shule ya msingi Uraki miti 500 ,washiriki 100 na Wanafunzi 200 tuliwapa Elimu ya utunzaji mazingira"alisema Nzali

Sambamba na hayo Baraza hilo limeweza kuendesha zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika mto Naura ,kwa umbali wa mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji kwa kuzingatia sheria ya usimamizi wa Mazingira ambapo bikoni 70 ziliwekwa kandokando ya mto huo.

Nzali amesema ni muhimu utunzaji wa mazingira kwa sababu ustawi wa mwanadamu na wa viumbe vyote, hutegemea hali nzuri ya mazingira ya asili wanayoishi ikiwa haitatunzwa, mazingira yanachafuliwa na hii hudhuru afya ya wanadamu na wanyama.

Aidha ikumbukwe kuwa siku ya Mazingira duniani huadhimishwa kila 5 juni ambapo Kimataifa itaadhimishwa nchini Sweden ambapo Kitaifa itafanyika Dodoma huku ikibeba Kauli mbiu isemayo "Dunia ni moja tu,Tunza mazingira" hakuna budi kuitunza,kwa hapa nchini Kauli mbiu "Tanzania ni Moja tu Tunza mazingira"

"Tutuze mazingira yetu " Tukiaharibu mazingira yetu tunaathiri uhai wetu,ni Wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu kwasababu mazingira ni uhai,kwani Tukiaharibu mazingira ni sawa na kiharibu makazi yetu"alisema.Nzali

Aidha Baraza hilo litaendelea kushiriki shughuli ambazo zimepangwa kwa kushirikiana na wadau wake ikiwemo usafi wa Mazingira maeneo mbalimbali ,kushuhudia maonyesho ya wadau kuhusu teknolojia ,ubunifu na mbinu za Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira katika Wilaya ya Arumeru ,pamoja na kuendelea kutoa Elimu kuhusu Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alisema , Serikali kupitia Ofisi ya Rais na ikishirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imeendelea kuratibu utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya upandaji na utunzaji wa miti inayotekelezwa nchini kwa kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

Aliyasema hayo wakati akiwaongoza wakazi wa Dodoma katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti katika mji wa serikali Mtumba,na kuiahiza timu ya wataalamu pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu kusimamia kikamilifu ujenzi wa mji wa serikali pamoja na programu ya upandaji miti pamoja na kuelimisha jamii juu ya upandaji bora wa miti kwa kuzingatia hali ya hewa ya eneo husika ili upandaji uwe na tija.

Aidha Maadhimisho hayo yalianza 27 mei 22 na kilele chake ni kirakuwa 5 juni 2022 ambapo Kimataifa itaadhimishwa nchini Sweden, chini ya Kauli mbiu isemayo "Dunia ni moja tu,Kauli ya Kitaifa ikiwa Tanzania ni Moja tu :Tunza mazingira"

"Hakuna budi ni lazima tutunze mazingira yetu " Tukiaharibu mazingira yetu tunaathiri uhai wetu,ni Wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu.alisema Nzali

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilianzishwa kwa Sheria ya Taifa ya Usimamizi wa Mazingira Na. 19 ya mwaka 1983 kama chombo cha kuishauri serikali juu ya masuala ya utunzaji endelevu wa mazingira,ambapo Baraza lilianza kazi rasmi mwaka 1986.

Sheria Na. 19 ya mwaka 1983 ilifutwa mwaka 2004 na Sheria ya Usimammizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 (Sura 191) ambayo ilianzisha Baraza kwa mara nyingine. Sheria hiyo mpya ililipa Baraza nguvu ya kisheria ya kusimamia hifadhi ya Mazingira nchini

Tangu kuanzishwa kwake Baraza hilo limekuwa likisimamia na kutoa ushauri kwa serikali kuhusu suala zima la hifadhi ya mazingira nchini, Kwa mujibu wa kifungu cha 17cha Sheria hiyo huku madhumuni ya kuanzisha Baraza hilo ni kuratibu utekelezaji wa sera na sheria ya mazingira katika nyanja kuu nne.

Nyanja hizo ni pamoja na Kutekeleza shughuli za uzingatiaji na usimamizi (enforcement and compliance) wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; Kusimamia mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) (Kuratibu, kufanya mapitio ya ripoti zaTAM kutoka kwa wenye miradi na kufuatilia utekelezaji wake); Kuwezesha ushiriki wa umma katika kufanya uamuzi unaohusu mazingira na Kusimamia kwa ujumla na kuratibu masuala yote yanayohusu mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Sheria nyingine zozote zilizoandikwa.

Aidha, kifungu cha 18 (2) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, inatoa mchanganuo mpana wa majukumu ya Baraza kama ifuatavyo:-Kufanya uhakiki wa mazingira (Environmental Audit), Kufanya tathmini ambazo zitasaidia katika kuhifadhi na kusimamia, Kufanya utafiti na kuratibu utafiti wa mazingira, kuchunguza, kutathmini na kukusanya taarifa na matokeo ya utafitina kuzisambaza kwa wadau, Kufanya mapitio na kutoa mapendekezo ili kuwezesha kupitishwa kwa taarifa/ripoti za TAM), Kuainisha miradi au programu zinazohitaji kufanyiwa ukaguzi na ufuatiliaji (Audit and Monitoring)

Kuhimiza na kuhakikisha usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya taifa katika utekelezaji wa sheria, Kuanzisha hatua madhubuti zenye lengo la kulinda na kudhibiti ajali zinazoweza kusababisha uharibifu wa mazingira na kubuni njia za kurekebisha maeneo ambayo yamepata uharibifu, Kutekeleza programu zenye lengo la kutoa elimu ya mazingira na kukuza weledi kwa kushirikiana na taasisi na sekta za wizara mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha usimamizi madhubuti na ushiriki wa jamii katika shughuli za kuhifadhi mazingira

Kuchapisha na kusambaza miongozo mbali mbali ya usimamizi wa mazingira inayolenga udhibiti wa uharibifu wa mazingira, Kutoa ushauri wa kitaalam na kusaidia taasisi na asasi mbali mbali zinazoshughulika na usimamizi wa maliasili na mazingira, na Kufanya shughuli nyingine zozote kwa maagizo ya Waziri wa Mazingira au kutokana na uhitaji wakati wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...