Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Jaji wa Mahakama ya haki wa za Binadamu Jaji Imani D. Daudi (katikati) wakifuatana na Viongozi wengine wakielekea katika Ukumbi wa Mikutano katika Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar Kufungua Kongamano la Mahakama za Kikanda na Kitaifa Barani Afrika.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakisimama wakati Wimbo wa Taifa kabla ya Ufunguzi wa Kongamano la Mahakama za Kikanda na Kitaifa Barani Afrika,leo katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa.
Baadhi ya Washiriki katika Kongamano la Mahkama za Kikanda na Kitaifa Barani Afrika,wakisikiliza kwa makini hotuba ya Ufunguzi iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar leo.
Jaji wa Mahkama ya haki Afrika Mashariki Mhe,Jaji Nestor Kayobera alipokuwa akisema machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi Kufunguwa Kongamano la Mahakama za Kikanda na Kitaifa Barani Afrika, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni ZanzibarRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Ufunguzi wa Kongamano la Mahakama za Kikanda na Kitaifa Barani Afrika,katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar, (kutoka kulia) Jaji wa Mahakama ya haki Afrika Mashariki Mhe,Jaji Nestor Kayobera,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mhe,Haroun Ali Suleiman na Jaji Mkuu Mteule Mhe.Jaji Khamis Ramadhan Abdalla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...